title : WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA
kiungo : WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA
WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA
Mkazi wa Morogoro, Frank Kisayo ameshinda zawadi ya televisheni ya kisasa aina ya Samsung yenye ukubwa wa inchi 32 kupitia promosheni ya Amsha Amsha Ushinde na Airtel Money ambayo inaendeshwa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.
Kisayo ambaye ni mkulima, alishinda televisheni hiyo kwenye droo ya tatu iliyofanyika kwenye Ofisi Makao Makuu ya Ofisi za kampuni ya simu ya Airtel jijini.
Akizungumza kwa njia ya simu mara baada kushinda droo hiyo, Kisayo alisema kuwa amefurahi sana kushinda zawadi hiyo yenye thamani si chini ya Sh750,000.
“Siamini kama nimeshinda, nasubiri kwa hamu zawadi yangu, naamini sasa suala la kununua televisheni kwangu limeisha baada ya kushinda zawadi hii nono ya droo ya Amsha Amsha,” alisema Kisayo.
Mbali ya Kisayo, pia Masoud Saleh wa Kisarawe na Shadrack Sanga wa Manyara kila mmoja alishinda simu ya mkononi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani Sh500,000.
Pia Eric Samwel ambaye ni mkazi wa Tanga alijishindia jezi na tiketi ya msimu ya kuona mechi ya Yanga na Simba za msimu ujao.
Maneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kuwa mpaka sasa washindi watatu wa televisheni, simu 25 na jezi 25 wamepatikana katika droo hiyo.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Dangio Kaniki, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Uhusiano Sabrina Msuya Kushiriki, mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.
Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Matukio Airtel Tanzania. Mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA
yaani makala yote WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/washindi-wa-amsha-amsha-ushinde-na.html
0 Response to "WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA"
Post a Comment