VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI.

VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI.
kiungo : VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI.

soma pia


VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI.



NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Madiwani na wakuu wa idara wanawake kutoka Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuwa na ujasili wa kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa maadili ya uongozi.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya maadili kwa viongozi wanawake, Kamishna wa Maadili  Mhe. Harold Nsekela, kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, amesema kuwa ni asilimia moja ya wanawake ndio wanaoshiriki katika kutoa taarifa ya ukiukwaji wa maadili.


Amesema kuwa kutokana utafiti uliofanywa na vikundi mbalimbali uliokuwa unapima ushiriki  wa utoaji wa taarifa umeonyesha wanawake kuwa na mwamko mdogo wa kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma.

Mhe. Nsekele amesema kuwa kutokana na hali hiyo, semina inaweza kuleta mabadiliko kwa kuwajengea uelewa viongozi wanawake katika mamlaka za serikali za mitaa kuhusu maadili ya viongozi wa umma.

"Baada ya kupata mafunzo wataweza kuwahamasisha na kuwaelimisha wanawake wezao katika ngazi ya kata na mitaa" amesema Mhe. Nsekela.

Ameeleza kuwa semina itawasaidia kuwa ujasiri kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika wanapokumbana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya viongozi wa umma.
Hata hivyo amefafanua kuwa majukumu ya msingi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ni pamoja na kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili, kupokea na kuhakiki matamko ya mali na madeni ya viongozi wa umma.

Majukumu mengine ni kufanya uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili pamoja na kutekelezaji wa majukumu ya utoaji wa elimu kwa ajili ya kukidhi dhima ya utawala bora kwa maendeleo ya taifa.



Hivyo makala VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI.

yaani makala yote VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/viongozi-wanawake-dar-wapewa-somo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIONGOZI WANAWAKE DAR WAPEWA SOMO UTOAJI TAARIFA UKIUKWAJI MAADILI."

Post a Comment