title : Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari
kiungo : Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari
Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari
Na Shamimu Nyaki-WHUSM,Dodoma.
Wananchi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Bonanza la michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ili kuunga mkono kauli mbiu ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kwa afya.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini hapo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza hilo lenye kauli mbiu ya "Karibu jiji la Dodoma, Michezo ni Afya" linatarajia kufanyika Julai 21 2018, katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.
"lengo la bonanza hili ni kuwakaribisha watumisha wa umma Jijini Dodoma na kuwalet a pamoja wananchi kwa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo ambukizi ".Alisema Bw.Singo.
Amezidi kufafanua kuwa mgeni rasmi katika Bonanza hilo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ambapo timu za Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bima ya Afya, LAPF, Chuo cha Mipango, Timu ya Mkoa wa Dodoma zimethibitisha kushiriki.
Bw. Singo ametoa rai kwa wadau wa michezo na wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika bonanza hilo ambalo litakuwa endelevu kwa kufanyika mara moja kwa mwezi .
Bonanza hilo litahusisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete, mazoezi ya viungo na mbio fupi.
Hivyo makala Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari
yaani makala yote Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wananchi-wa-dodoma-watakiwa-kujitokeza.html
0 Response to "Wananchi wa Dodoma watakiwa kujitokeza na kushiriki Bonanza la Wizara ya Habari"
Post a Comment