title : MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI
kiungo : MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI
MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI
Na WAMJW- Mwanza
Mabaraza ya Watoto nchini yamehimizwa kutumia elimu wanayoipata kuibua vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili kuondokana na vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza alipowatembelea na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.
Dkt.Ndugulile amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 takribani wanawake na watoto 41,000 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kati yao 13,000 wakiwa ni watoto pekee.
Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili vimeongezeka ukilinganisha na matukio ya vitendo vya ujambazi nchini ambapo suala hilo halitakiwi kufumbiwa macho na wananchi na wadau.
Aidha Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa wananchi hasa wazazi na watoto kutomalizana nyumbani endapo vitatokea vitendo vya ukatili katika familia zao bali kuviripoti katika mamlaka husika.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akihojiwa na wanahabari watoto wa mkoa wa Mwanza wakati alipowatembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Joel Festo akiishukuru Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali watoto kuanzia katika utoaji wa huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akimkabidhi Mtunza Hazina wa Baraza la watoto la Mkoa wa Mwnzxa kiasi cha Shillingi 250,000/= ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ununuzi wa printa kwa ajili ya shughuli za ofisi za Baraza hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kitaifa wa Baraza la Watoto na Viongozi na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza, viongozi wa mkoa na wadau wa watoto mkoani humo mara baada ya kulitembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI
yaani makala yote MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mabaraza-ya-watoto-yahimizwa-kufichua_18.html
0 Response to "MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI"
Post a Comment