title : WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO
kiungo : WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO
WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
SERIKALI ikiwa inaendelea uwekaji wa mifumo ya utoaji huduma kwa njia ya kielekroniki katika taasisi zake kwa upande wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umepiga hatua kubwa katika hilo katika kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wananchi zinakidhi haja zao.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Ofisa Habari wa RITA Jafari Malema amesema mifumo hiyo ya kielekroniki ni ya Usajili wa Vizazi na vifo unaojulikana kama Birth Registration Fourth Generation (BRS4), Mfumo wa malipo ya ada ya huduma wa Serikali, Government elecronic Payment Gateway (GePG) na Mfumo wa Uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu na watu wengine.
Malema ameeleza kuwa "Kwa kuwa mwaka jana tulipata changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi kufikika katika ofisi zetu na kusababisha msongamano ndiyo maana mwaka huu tumekuja na suluhisho la kudumu na tumefanikiwa kwa asilimia 98 ya uhakiki na kuwajibu wanafunzi," ameeleza.
Ameeleza hadi sasa wamepokea jumla ya maombi 95,561 kati ya hayo maombi 94,344 sawa na asilimia 99 yamefanyiwa kazi na kujibiwa na maombi 1217 sawa na asilimia 1.3 yanaendelea kufanyiwa kazi na kati ya maombi yote yaliyojibiwa ni maombi 92,304 sawa na asilimia 98 yamehakikiwa na hayana mapugufu yoyote na maombi 2040 sawa na asilimia 2 yameonekana kuwa na mapungufu na yanafanyiwa marekebisho.
Akieleza utofauti wa kiutendaji kwa sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo huduma zilitolewa kwa mifumo ya kizamani ya karatasi, Malema ameeleza kuwa mfumo huo umekuwa rahisi zaidi katika utoaji wa huduma ukilinganisha na miaka iliyopita kwani huduma zote hufanyika kwa njia mtandao wanachotakiwa ni kutembelea tovuti ya http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki.
Afisa Mawasiliano wa (RITA) Jafari Malema akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Wananchi kuwasilisha nyaraka halisi na kuacha kutumia nyaraka bandia ambazo hazitoki (RITA).Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
Afisa Mawasiliano (RITA) Jafari Malema kushoto na Afisa Masoko RITA, Edwin Mbekenga, wakionesha vyeti feki vya kuzaliwa.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Maofisa wa (RITA) wakiendela na kazi ya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa
Makao Makuu jijini Dar as Salaam.
Hivyo makala WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO
yaani makala yote WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wanafunzi-waipongeza-rita-uhakiki-wa.html
0 Response to "WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO"
Post a Comment