title : WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA
kiungo : WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA
WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wakulima wa Wilaya ya Kibiti wazidi kuneemeka na bei ya ufuta! katika mnada wa nne (4) kwa msimu huu ambapo bei ya ufuta kwa kilo imepanda kufikia sh. 3,300 kutoka sh. 3,100 ya mnada uliopita wa tarehe 19 Julai na huku bei ya chini ikiwa sh. 3,110.
Wakati huo huo ufuta ghalani umepanda kufikia tani 582.5 kutoka tani 454.8 za mnada uliopita.
Kwa ujumla wananchi wa Kibiti wameendelea kuishukuru serikali kwa kufanya maamuzi ya kuwakomboa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao kwa mara ya kwanza ufuta umekuwa wa manufaa makubwa kwa mkulima. Akifungua mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mh.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu alisema hatamvumilia yeyote atakayejaribu kuuharibu ama kuuvuruga mfumo unaoendelea wa mauzo ya ufuta kwa stakabadhi ghalani ikiwa ndiyo maagizo ya serikali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo bibi Alvera Ndabagoye alipongeza hatua iliyofikiwa na ushirikiano mzuri uliopo pande zote ambao umekuwa wa manufaa si tu kwa mkulima bali hata kwa wafanyabiashara wenyewe na serikali kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mh. Gulamhussein Kifu akihutubia katika mnada huo uliofanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya .
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti Milongo Sanga akizungumza katika mnada huo uliofanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya .
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kibiti Alvera Ndabagoye akizungumza katika mnada huo
Watunza funguo Afisa Ushirika wa Wilaya na Mwenyekiti wa AMCOS ya Kibiti wakifungua sanduku la tenda.
baadhi ya wafanyabiashara, wakulima na watumishi waliohudhuria mnada huo.
Hivyo makala WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA
yaani makala yote WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wakulima-wan-ufuta-kibiti-wazidi.html
0 Response to "WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA"
Post a Comment