Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri

Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri
kiungo : Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri

soma pia


Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri

Frank Mvungi- MAELEZO, Handeni
Serikali Wilayani Handeni imewataka wananchi kutumia fursa ya kujengwa kwa Kituo cha umahiri katika Wilaya hiyo kujiletea  maendeleo kupitia sekta ya madini.
Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na Wizara ya Madini kupitia mkandarasi ambaye ni SUMA JKT,  Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe amesema hiyo ni fursa  adhimu kwa wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuwa watajengewa uwezo wa namna bora ya kushiriki katika uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta hiyo.
“Wananchi sasa hawatahitaji kusafiri kwenda mikoa mingine kujifunza namna ya kuchimba madini, kuchenjua na hata kushiriki katika kuendeleza sekta hii kwa kuwa kituo cha umahiri  ( Centre of  Excellence) kinajengwa hapa Handeni hivyo ni jambo la kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwainua wachimbaji wadogo kwa kuwaongezea ujuzi” Alisisitiza Mhe. Gondwe.
Akifafanua Gondwe amesema kuwa Wilaya hiyo ina hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali ambayo hayajachimbwa hivyo ujenzi wa kituo hicho utasaidia katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo na kuwainua wananchi kwa kuwa watachimba madini hayo kwa kuzingatia sheria ikiwemo kulipa kodi zote na hivyo kuondoa tatizo la uwepo wa wachimbaji wasiozingatia weledi na sheria ya madini.
Wizara ya Madini inayotekleza mradi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw. Godwin Gondwe akisisitiza umuhimu  wa Kituo cha umahiri  kwa wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Handeni kinachojengwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuinua wachimbaji hao katika Wilaya hiyo na maeneo yote ya mikoa ya jirani na Wilaya hiyo.
 Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)akipokea ramani ya Kituo cha umahiri (Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa niaba ya meneja wa ujenzi wa SUMA JKT Kanda ya Kaskazini Meja. Daudi Zengo  kutoka kwa Mshauri muelekezi wa mradi huo Bw. Beno Matata kutoka Kampuni ya Inter Consult Ltd, mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini katika Wilaya ya Handeni, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya Inter Consult Ltd Bw. Beno Matata akieleza mikakati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa inasimamia mradi huo wa ujenzi wa Kituo cha Umahiri kitakachowanufaisha wachimbaji wadogo kinachojengwa Wilayani Handeni ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinua wachimbaji hao.
 Mjiolojia wa Wizara ya Madini Bi. Veronica Nangale akisisisitiza jambo  kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (hayupo pichani) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kabla ya hafla ya kukabidhiwa kwa eneo kitakapojengwa kituo  cha umahiri(Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini, hafla hiyo ilifanyika Wilayani Handeni, ujenzi wa kituo hicho unafanyika kupitia  Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.
 Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhiwa eneo na ramani ya Kituo cha Umahiri kwa wachimbaji wadogo wa madini kinachojengwa na mkandarasi SUMA JKT, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Madini kuimarisha sekta hiyo na kuwainua wachimbaji wadogo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri

yaani makala yote Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wachimbaji-wadogo-handeni-kunufaika-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri"

Post a Comment