title : RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF
kiungo : RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF
RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF
Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, amewaonya Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za mkoa huo ambao watakalia fedha za wananchi wanaojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa na kuzitumia vinginevyo wanawajibishwa mara moja.
Dk Kebwe alisema hayo, wakati akifunga kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya Mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro mwanzoni mwa juma hili mjini hapa.
Wajumbe wa kikao hicho walipitia taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Tuimarishe Afya kunzia Juni hadi Novemba 2017 pamoja na utekelezaji wa Mradi ya mkoa wa Juni hadi Novemba mwaka huu uliohusu mpango wa uchangaji wa CHF iliyoboreshwa na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali.
Dk Kebwe aliwataka wakurugenzi hao wanapopelekewa makusanyo ya fedha za kaya zinazotokana na wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa, wajibu ni kuziingiza kwenye mfumo na kuzipeleka kwenye vituo ili zikatumike kununua dawa na vifaa tiba na si vinginevyo.
Pamoja na kusema hayo ,aliishukuru Serikali ya Uswiss kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la nchi hiyo kwa ufadhili wa mradi wa Tuimarishe Afya ambao unachochea uboreshaji wa huduma za afya kupitia mpango wa CHF iliyoboreshwa unaotekelezwa katika mikoa mitatu ya Shinyanga, Dodoma na Morogoro.
Naye Meneja mkoa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) , Dk Harun Machibya alisema kuwa kiwango cha kujiunga na CHF iliyoboreshwa kimkoa imeongezeka kutoka asilimia 3 tangu kuanza kwa mradi huo na kufikia asilimia 11.3 hadi Novemba mwaka huu na mwekezo mzima ni kifikisha asilimia 25 hadi Julai 2018.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa huo, Clifford Tandari alizitaka halmashauri ambazo zinadaiwa fedha na Hospitali ya Rufaa ya mkoa kuwasilisha malipo yao mara moja ili huduma za wananchi ziweze kupatikana kwa ufanisi mkubwa.
Hata hivyo alisema , siku za usoni mpango huo unaunganishwa kiteknolojia kwa kaya kuweza kujiunga kuwa wanachama wa CHF iliyoboreshwa kupitia mifumo ya miamala ya fedha kwa njia ya simu kama ilivyo kwa huduma nyingine za kifedha .
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe,akisisitiza jambo wakati wa kufunga kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro wengine waliokaa kwenye meza kuu ni Katibu Tawala wa mkoa , Clifford Tandari pamoja na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo.
Meneja wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) , Manfred Stoemer ( kulia) akiteta jambo na Kiongozi wa Wataalamu wa Mradi huo, Profesa Manorios Meshack ( kushoto) wakati wa kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro wakisiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ugufaji wa kikao hicho kilichofanyika mkoani Morogoro.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro ( mstari wa mbele ) ambao ni wajumbe kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi ya ugufaji wa kikao hicho kilichofanyika , mkoani Morogoro.
Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Frank Jacob akisoma sehemu ya maazimio ya kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro kabla ya mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wapili kulia walioketi ) kufunga kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mradi wa Tuimarishe Afya wa mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro kilichofanyika mkoani Morogoro.( Picha na John Nditi).
Hivyo makala RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF
yaani makala yote RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rc-morogoro-aonya-wakurugenzi.html
0 Response to "RC MOROGORO AONYA WAKURUGENZI WANAOKALIA FEDHA ZA CHF"
Post a Comment