title : VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019
kiungo : VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019
VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza mkakati wake katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 ambapo amesema kuwa huduma kama afya, elimu na miundombinu ni muhimu na lazima jimboni humo.
Akizungumza na Michuzi blog Gulamali emeeleza kuwa vijiji vyote vya jimbo la Manonga vitapata umeme mwaka huu wa fedha 2018/2019.
Kuhusu huduma za afya Manonga amesema kuwa wamefanikiwa kujenga kituo cha afya kilichogharimu Sh. milioni 400 na hiyo ni katika kuwasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kituo hicho kina jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mama na mtoto, maabara ya kisasa, jengo la kufulia na nyumba ya mganga katika kituo cha afya Simbo.
Aidha ameeleza wanaelekea kupata shule ya kwanza jimbo la Manonga na shule 3 Wilaya ya Igunga kuwa na kidato cha 5 na 6 kwani hadi sasa mabweni 4 na madarasa 2 kwa ajili ya kidato cha tano na sita yamekamilika katika shule ya Sekondari Ziba.
Kuhusu ujenzi wa daraja la Manonga kutoka Choma kwenda Shinyanga ambalo limekuwa ni kilio kwa miaka 50 Gulamali ameeleza kuwa wamepata zaidi ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.Aidha ameeleza kiwanda cha pamba cha Manonga kilichokufa kwa miaka 20 kimefufuliwa na kinatoa ajira zaidi ya 500 kwa vijana wa Igunga, Tabora na nchini kwa ujumla na hii ina inatoa fursa kwa wajasiriamali hasa mama ntilie kwa kupata kipato kutokana na huduma wanazozitoa.
Kuhusu mradi mkubwa wa maji kutoka Mwanza hadi Igunga Gulamali ameiambia blogu ya jamii kuwa zaidi ya dola milioni 265 za kimarekani zimetengwa kwa ajili kutekeleza mradi huo na vijijji na kata zitapata maji kupitia mradi huo pia vijiji vya Mwisi, Mwamala na Sungwizi vitapata maji kutoka fedha kiasi ya Milioni 600 iliyotengwa kwa ajili ya mradi wa maji.
Gulamali ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa zinazotolewa hasa katika elimu kwa kuwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii kwani kama serikali wamewekeza sana katika elimu na watahakikisha wanatengeneza mazingira bora katika upatikanaji wa elimu bora.

Hivyo makala VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019
yaani makala yote VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/vijiji-56-manonga-kupata-umeme-mwaka-wa.html
0 Response to "VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019"
Post a Comment