title : JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili
kiungo : JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili
JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amesema Kiswahili kinachozungumzwa Zanzibar ndio Kiswahili fasaha zaidi kuliko cha mataifa mengine hivyo ameitaka Jumuiya ya Uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili Zanzibar (JULUKIZA) kuendelea kukikuza.
Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo wakati alipokuwa akizungumza na wana jumuiya hiyo ambayo imetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa na kuzindua kitabu kipya kilichopewa jana la ‘Mjue Chimbeni bin Kheir’ kilichotungwa na Bibi Mwanakombo Mwadini Sheha, ambae ni mwanachama wa Jumuiya hiyo.
Alisema lafdhi ya Lugha ya Kiswahili cha Zanzibar ni nzuri zaidi tangu zamani na ndio sababu vituo vingi vya Redio za nje zinazoanzisha matangazo ya lugha ya Kiswahili watangazaji walikuwa wakitoka Zanzibar na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwenye vituo hivyo.
Ayoub alisema katika Barani la Afrika Lugha ya Kiswahili inashikilia nafasi ya kwanza kuzungumzwa na kinashika nafasi ya sita kuzungumzwa duniani kote na hii yote inatokana na umuhimu wake.
Amewataka Wanajumuiya kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na sekta binafsi katika kuikuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuwapa busara ya kukienzi Kiswahili kwani ni urithi wetu.
Hata hivyo amewataka Wasani wa sasa kuwa na mashirikiano katika kufanya kazi zao na kuungana na wasanii wa zamani kwani nao ni muhimu katika kukikuza na kukilinda Kiswahili.
Nae mjumbe wa JULUKIZA Dhalha Mohamed Muhsin akisoma risala amesema utamaduni wa mswahili unatokana na lugha ya Kiswahili hivyo amezitaka asasi za kiraia kutoa mchango wao kuhakikisha Kiswahili kinalindwa na kukuzwa ili kiwe moja ya chanzo cha ajira kwa wazanzibari.
Aidha amesema Jumuiya ya uendelezaji lugha ya kiswahili Zanzibar itahakikisha inachukua juhudi mbalimbali katika kuona lugha ya kiswahili inakuwa na kuenea zaidi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha utamaduni wa Mzanzibari usipotee.
Dhalha amesema harakati za kukikuza kiswahili zinaendelea katika jumuiya hiyo ikiweno kuandaa majarida, makongamano na mafunzo ya lugha katika mataifa mbalimbali ili kusaidia jamii kuona umuhimu wa Kiswahili.
Akitoa changamoto zinazowakabili katika jumuiya hiyo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama projeta , ajira kwa vijana waliosoma katika jumuiya hiyo na tayari wamepata shahada ya Kiswahili na Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwasaidia projeta .
Kwa upande wake Mshauri wa Rais katika masuala ya Utamaduni Chimbeni Kheri aliwashukuru wanajumuiya hiyo na kusema kazi ya Sanaa ameanza muda mrefu na amewaomba wasanii wachanga kuendeleza fani hiyo ili iweze kuibua vipaji vyao.
Aliikumbusha hadhiri iliyiohudhuria uzinduzi wa kitabu na maadhimisho hayo michezo aliyoigiza na kumpatia sifa kubwa kuwa ni pamoja na Talaka mpe jirani, Nia safi hairogwi na nyimbo ni Kibali inayoghaniwa na Bi. Mwanacha Hassan na You are all well come to Zanzibar the Spice Island aliyoimba yeye mwenyewe.
Mwisho
Hivyo makala JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili
yaani makala yote JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/julukiza-yatakiwa-kukikuza-kiswahili.html
0 Response to "JULUKIZA yatakiwa kukikuza Kiswahili"
Post a Comment