title : UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU
kiungo : UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU
UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU
LATIFA Mohammed Ngea kutoka Zanzibar ameibuka kidedea katika tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu na kupata hundi ya shilingi milioni 3.
Latifa ni miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.Latifa alipata tuzo hiyo kwa kubuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo.
Mfumo huo unaojiendesha wa umwagiliaji maji unaweza kutumia king’amuzi ili kubaini wapi pana unyevu na wapi pakavu ili maji yaweze kupelekwa.Tangu kuanza kwa maonesho hayo takribani wiki sasa, wageni mbalimbali wamepata nafasi ya kuona ubunifu wa vijana hao katika roboti, sanaa na kilimo.Aidha walionesha ubunifu wao unavyofanyakazi sanjari na kauli mbiu ya sabasaba mwaka huu inayosema “Kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda”.
Baada ya wananchi kuwasikiliza wabunifu wote watatu, wageni walipata fursa ya kupiga kura nani waliamini alionyesha ubunifu bora zaidi, ndipo Latifa alipoibuka mshindi.Mbunifu mwingine alikuwa ni Gracious Fanuel anayetoka mkoani Kilimanjaro alipata ushindi wa pili.
Huyu yeye alitengeneza roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani.Roboti aliyotengeneza ni mfano wa Mkono ambao unaweza kuendeshwa kwa simu ya mkononi na anatarajia kukuza ubunifu wake ili ufikie hatua ya kuwa na mkanda wa uzalishaji bidhaa na pia kusaidia watu wenye ulemavu.
Mbunifu mwingine ni Amos Mtambala, kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali yeye alishika nafasi ya tatu. Amos alipata mafunzo kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) na tangu hapo amekuwa akipanua mtandao wake na kuwachukua zaidi ya vijana 100 ambao hutengeneza kazi za sanaa na kuuza nchini na pia kimataifa.
Zaidi ya watu 500 katika Viwanja vya Sabasaba na kupitia mitandao ya kijamii walipiga kura kwa kijana yule wanayeamini aliandaa ubunifu bora zaidi.Mshindi wa kwanza alipata shilingi milioni 3 huku mshindi wa pili akipata shilingi milioni 2 na wa tatu shilingi milioni 1.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu kwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar aliyebuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati), mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) huku wakiwa wameshikilia hundi zao.

Hivyo makala UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU
yaani makala yote UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/un-yatunuku-ubunifu-katika-maendeleo.html
0 Response to "UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU"
Post a Comment