Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP

Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP
kiungo : Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP

soma pia


Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP

MKUU wa mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga  amesema serikali ya Tanzania inafurahishwa na namna Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyofanya kila linalowezekana kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao ndio wenyeji wa wenzao wanaokimbia matatizo nchi jirani.
Akizungumza katika mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP), alisema kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo ikiwamo ya kupeleka ushawishi kwa wadau wa maendeleo ya kusaidia wananchi wa Kigoma wakiwemo wageni wakazi na wakimbizi.
Akiwa Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo, Maganga alisema pamoja na juhudi hizo bado mkoa una changamoto nyingi zinazotakiwa kushughulikiwa japo serikali imeendelea na juhudi za kuboresha mazingira ya miundombinu ya kuwezesha shughuli za kiuchumi.
Alisema toka mkutano wa mwisho mwaka jana, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kampeni za serikali za kuufungua mkoa huo kiuchumi kwa kutengeneza miundombinu mbalimbali kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara.
Alisema serikali inaendeleza miradi ya kimkakati hasa ya barabara zinazounga mkoa huo na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC)  na mikoa mingine ya Tanzania ya Shinyanga, Mwanza, Kagera na Tabora.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (wa pili kulia)akizungumza wakati akifungua mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford (kushoto).
 Kansela wa Ubalozi wa Norway, Britt Kjolas akitoa salamu kwa niaba ya wadau wa maendeleo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha akiwasilisha rasimu ya makubaliano ya utekelezaji wa Programu ya KJP wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mchambuzi  Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho
 Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) nchini, Stephanie Shanler akiwasilisha hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi wa KJP eneo la kuzuia ukatili kwa wanawake na watoto wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Viola Kuhaisa akiwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa eneo la elimu wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) wakiwemo wadau wa maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP

yaani makala yote Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tanzania-yafurahishwa-na-un-katika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP"

Post a Comment