title : Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima
kiungo : Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima
Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima
Mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku serikali ikiahidi kushirikiana na wadau wa mchezo huo kuhakikisha unachezwa maeneo yote nchini ili utumike kutangaza sekta ya utalii zaidi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda alisema mashindano hayo yameonesha wazi kuwa endapo mchezo huo utasambaa zaidi katika maeneo yote hapa nchini yatavutia zaidi washiriki kutoka mataifa mbalimbali ambao pia watakuja kama watalii.
“Ni kupitia mashindano haya ndio nimeweza kugundua nguvu ya mchezo wa golf katika kutangaza utalii kwa sababu umeweza kuwavutia washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ni bahati mbaya tu kwamba kwasasa mchezo huu unachezwa kwenye mikoa michache sana hapa nchini tena ukitafsiriwa kuhusisha tabaka flani jambo ambalo si kweli,’’ alisema.
Aliongeza kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge yanakuwa ya kimataifa ili yavutie zaidi washiriki kutoka mataifa ya nje.
Mashindano hayo ya siku tatu yaliandaliwa na serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na yalihusisha washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wachezaji wa kulipwa yaani ‘Professionals’ na washiriki wa kawaida yaani ‘Amateurs’ ambapo mchezaji Aidani Nziku kutoka klabu ya Golf ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam akiibuka mshindi wa jumla.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda (alieva jaketi la kaki) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 , mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela
Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda akionyesha ufundi wake kwenye mchezo huo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela nae akionyesha utaalamu wake kwenye mchezo huo.
Kapteni wa klabu ya Golf ya Mufindi Bw Glyn akionyesha umahili wake kwenye mchezo huo mbele ya wageni waalikwa.
Hivyo makala Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima
yaani makala yote Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/serikali-yaahidi-kuufikisha-mchezo-golf.html
0 Response to "Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima"
Post a Comment