BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu

BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu
kiungo : BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu

soma pia


BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu

Na Beatrice Lyimo-Maelezo, Dodoma
Serikali imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma (PSSSF) kuanzia Agosti 1, mwaka huu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametangazaa leo jijini Dodoma.
Mhe. Mhagama amesema kuwa Serikali imekamikisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake, na kwamba kutokana na hatua hiyo wafanyakazi wote watakaoajiriwa katika sekta ya umma watasajiliwa katika Mfuko wa PSSSF na wale watakaoajiriwa katika sekta binafsi watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF.
"Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF", alisisitiza mhe. Mhagama
Waziri Mhagama kaongeza kuwa Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.
Akizungumzia rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa  Waziri Mhagama amesema itahamishiwa katika Mfuko mpya wa PSSSF. Pia Waziri Mhagama amewatoa hofu ya kupoteza ajira watumishi wote wa mifuko iliyounganishwa  kwa kuwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa taasisi.
Amesema ili kuondoa sintofahamu Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) imeandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria na kanuni za PSSSF ili kuhakikisha kwamba wanachama na wadau wote wa sekta ya hifadhi ya jamii wanakuwa na uelewa sahihi wa sheria hizo na mabadiliko yaliyofanyika.
Mbali na hayo, Waziri Jenista ameteua wajumbe wa Bodi ya Mfuko huo ambao ni Bi. Leah Ulaya, Bw. Rashidi Mtima, Dkt. Aggrey Mlimuka, Bi. Stella Katende, Bw. Thomas Manjati, Bw. Henry Katabwa, Bi. Suzan Kabogo pamoja na Bw. Jacob Mwinula.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitangaza rasmi leo Jijini Dodoma tarehe ya kuanza  kufanya kazi kwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo mfuko huo unaanza kazi Agosti Mosi mwaka huu.Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera na Uratibu Prof. Faustine Kamuzora.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF)  unaanza kutekleza majukumu yake bila kuathiri huduma kwa wanachama wa mifuko iliyounganishwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma  (PSSSF) Bw. Eliud Sanga (katikati) akisisitiza kuhusu hatua watakazochukua kuhakikisha kuwa mfuko huo mpya unatatua changamoto zilizokuwepo awali katika mifuko iliyounganishwa kuunda mfuko huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza tarehe ya kuanza rasmi kufanya kazi kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa  Watumishi wa Umma(PSSSF) leo Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa SSRA Dkt. Irene Isaka. Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO


Hivyo makala BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu

yaani makala yote BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/breaking-newssss-mfuko-mpya-wa-hifadhi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu"

Post a Comment