Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake

Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake
kiungo : Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake

soma pia


Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake



Hussein Ndubikile, 
Mwambawahabari
Mkazi  wa Mtaa wa Mamboleo B  wilayani Temeke,  Joseph Liapinda (84) amemsifu na kusimulia jinsi aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, ambaye kwa sasa ni Mbunge  Muleba Kusini  mkoani Kagera (CCM), Profesa  Anna Tibaijuka  alivyomsaidia kuokoa nyumba  yake iliyotaka kudhulumiwa.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee alipokutana na Profesa Tibaijuka katika  kuuaga Mwili wa aliyekuwa  Mbunge wa Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Stephen Ngonyani ‘ Profesa Maji Marefu’ (CCM).

Liapinda amesema mwaka 2014 nyumba yake iliyoko Kata ya Sandali wilayani humo ilitaka kudhulumiwa na mtu aliyemruhusu kukaa bure kwa makubaliano ya kujenga choo akishirikiana na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo.

Amebainisha kuwa  mtu aliyekuwa akikaa kwenye nyumba yake hakujenga choo na mwenyekiti wa mtaa huo akishirikiana na mjumbe  wa nyumba kumi, Josephina Francis  walimpa namba feki ya nyumba iliyomwekeza kuwa sio yake.

Amesisitiza kuwa baada ya kufanyiwa kitendo hicho alianza kupigania haki yake kwa kwenda Makao makuu ya wizara husika ndipo alipokutana na Profesa Tibaijuka na kumueleza mkasa mzima ambapo Mbunge huyo alimpa barua yenye maelekezo iliyomtaka aende kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye  sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe  Chiku Galawa.

Amefafanua kuwa baada ya kwenda kwa mkuu wa wilaya huyo na kwamba yule aliekuwa amempa hifadhi katika nyumba yake alikamatwa na kuweka ndani na kurudishiwa nyumba hiyo katika himaya yake.

Amemshukuru Profesa Tibaijuka kwa kusema bila msaada wake nyumba yake asingeipata na kwamba anaishi na familia yake ya watoto sita pamoja na mkewe.

Kwa upande wake, Profesa Tibaijuka amempa shukrani mkazi huyo kwa kutambua mchango wake uliofanikisha kuokoa nyumba yake kwa wadhulumati na kumsisitiza aendelee kuishi kw amani.

Katika hatua nyingine, Profesa  Tibaijuka amesema ameupokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Maji Marefu kwa kuwa alikuwa ni mtu msikivu, mwelewa na mjenga hoja bungeni.
“ Ni masikitiko makubwa Maji Marefu namfahamu  alikuwa mbunge mwelewa na mjenga hoja tulipokuwa bungeni, “ amesema.


Hivyo makala Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake

yaani makala yote Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mzee-liapinda-amfagilia-profesa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mzee Liapinda amfagilia Profesa Tibaijuka asimulia jinsi alivyomsaidia kuipata nyumba yake"

Post a Comment