BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU

BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU
kiungo : BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU

soma pia


BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka  ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuuwezesha mkoa wa Simiyu katika kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia miradi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani humo.

Bw. Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umejipanga kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na TADB ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha wakulima wanalima kisasa ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.

Bw. Mtaka aliongeza kuwa Mkoa wa Simiyu uko tayari kufanya kazi na Benki ya Kilimo kupitia vikundi vya uzalishaji, Halmashauri na Miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo, ikiwa ni pamoja na miradi ya mfano ya umwagiliaji ya Mwamanyili Wilayani Busega  ulio katika hatua ya upembuzi yakinifu na Mwasubuya wilayani Bariadi ambao uko katika hatua ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

“Tungehitaji kuwa Mkoa ambao kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo tungetengeneza namna ambayo ingewasaidia wakulima na ikasaidia mikoa mingine kuja kuona maendeleo ya kilimo  ambayo ni matokeo ya Serikali kuwekeza katika Benki ya Kilimo” amesema Mtaka.

"Sisi kama Mkoa tumejipanga, tumetoa Elimu ya utayari na
namna ya utekelezaji wa shughuli zote kwa wataalam wetu pamoja na wananchi na isitoshe tayari tumeshafanya utafiti na kuandaa mwongozo wa uwekezaji ndani ya mkoa, hivyo tunawakaribisha kuwekeza,” aliongeza.
Aidha, Bw.Mtaka ameongeza kuwa Mkoa wa Simiyu unatekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo hadi sasa kuna kiwanda cha chaki na maziwa na miradi mingine minne ya viwanda iko katika upembuzi yakinifu.
 Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akizungumza wakati walipofanya ziara ya kujionea miradi ya kilimo mkoani Simiyu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kilimo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) kuhusu nafasi ya TADB katika kuwasaidia wakulima nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Kilimo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya uongozi wa Mkoa huo, wataalam wa kilimo, mifugo na ushirika na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kilimo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU

yaani makala yote BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/benki-ya-kilimo-yaaswa-kuwezesha-miradi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BENKI YA KILIMO YAASWA KUWEZESHA MIRADI YA MAENDELEO SIMIYU"

Post a Comment