title : Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa
kiungo : Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa
Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa
WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani, amezindua umeme wa gridi ya Taifa Wilaya ya Muleba, ambapo alisema kuwa hatua hiyo sasa inakwenda kuifanya wilaya hiyo kuwa na umeme wa uhakika.
Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa umeme huyo wa gridi ya Taifa ulifanyika katika Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba, Dk. Kalemani, amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania hasa wa maeneo ya vijijini wanapata umeme kwenye nyumba zao.
Amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa KV 33 wa umeme wa gridi ya Taifa kutoka Wilayani Chato, Rais Dk. John Magufuli, aliridhia na kutoa Sh milioni 778 ili kuweza kukamilisha kazi hiyo.
Kutokana na hali hiyo Waziri Dk. Kalemani, amesema kuwa mkakati wa Serikali kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye umeme wa gridi ya Taifa ambao ni wa uhakika katika kufanikisha uchumi wa viwanda kwa kjuwa na nishati ya uhakika na yenye usalama.
“Kuzinduliwa kwa umeme huu wa gridi ya Taifa sasa kuzifanya Wilaya za Muleba, Biharamulo na Ngara sasa kuwa na umeme wa uhakika wa hapa nchini kwetu. Tena umeme huu ni salama zaidi maana awali tulikuwa tunategemea umeme kutoka kwa wenzetu nchi ya Uganda jambo ambalo hata wakizima kule hatuna la namna ya kuuliza.
“Na ninafuraha kubwa kuwaambia kwamba mkataba wa kazi hii ya ulikuwa ni wa miezi miwili ambapo Juni 2, mwaka huu ulisaini na kuwekeana malengo kwamba hadi kufikia Agosti 2, mwaka huu kazi hii iwe imekamilika. Lakini leo (jana) ninafuraha kuona kazi hii imekamilika wiki moja kabla ya muda wa mkataba,” amesema Dk. Kalemani
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akishangilia baada ya kuzindua umeme wa gridi ya Taifa katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera leo.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo, wakati wa uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa wa KV 33 ambapo sasa Wilaya ya Muleba, Biharamulo na Ngara zitakuwa zinatumia umeme huo.
Waziri wa Niashati, Dk. Kalemani, akiwashukuru mafundi waliofanikisha ujenzi znjia za umeme wa gridi ya Taifa baada ya kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Hivyo makala Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa
yaani makala yote Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/muleba-yaunganishwa-rasmi-umeme-gridi.html
0 Response to "Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa"
Post a Comment