title : MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA
kiungo : MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA
MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA
MwambawahabariMkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amefanikisha kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro wa eneo la soko lililopo eneo la Tabata Liwiti uliodumu kwa miakamingi.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Mjema amesema kuwa eneo hilo ni la Manispaa ya Ilala na ramani yake inaonyesha Kuna soko, na kusema kuwa hakufurahishwa na barua iliyotolewa na Afisa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, aliefahamika kwa jina la Edger ambapo aliruhushu bila kuzingatia Ramani za manispaa akaruhusu upande wapili kuchukua eneo hilo.
"Hatukufurahishwa na barua ya Ediger yeye alitoa barua kama yeye badala ya kusikiliza pande zote na hakushirikisha Manispaa tarehe 11/4/2018 tuliandika barua kupinga uamuzi huo tukaleta ofisini kwako" amesema
Amesema Mgogoro huo uliendelea kushika kasi pale ambapo Mwezi Juni kulitokea mgogoro na fujo kubwa Jambo ambalo alilazimu kutuma polisi kupitia RPC Buguruni na kutuliza ghasia na kumkamata na walio chochea fujo hiyo wakapelekwa polisi kwa mahojiano.
Aidha baada ya kikao alifanya maamuzi nakusema kuwa eneo hilo litabakia kuwa eneo la soko na kuitaka Manispaa kumtafutia eneo lingine mwananchi ambaye alikuwa anadai kuwa lake .
"Baada ya Manispaa kujiridhisha kuwa ni eneo la soko Tulitulia kwa muda na huyo mama ambaye alisema ni mjane tulimwambia kuwa sisi hatumnyimi kama anahaki yake atatafutiwa eneo jingine" alisema
Ameongeza kuwa wakati wanafanya hayo maamuzi akatokea mtu aliye sema ni Mwekezaji amenunua eneo hilo kabla uamuzi haujatolewa ndipo tukaita mkutano ukimuhusisha Mkuu wa mkoa hii leo.
Hata hivyo mgogoro huo umemalizika leo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda baada kusikiliza wananchi na Manispaa ya Ilala na kutoa maamuzi kuwa eneo hilo liendelee kutumika na kuwa chini ya Manispaa , na mwananchi anaye dai apewe eneo lingine.
Kwa upande wao wananchi wa wa eneo hilo wameshukuru kuisha kwa mgogoro huo na kuahidi kwa wataendelea na shughuli zao za soko.
Hivyo makala MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA
yaani makala yote MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/morogoro-wa-soko-liwiti-watatuliwa.html
0 Response to "MOROGORO WA SOKO LIWITI WATATULIWA"
Post a Comment