title : MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA
kiungo : MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA
MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Raia wa Marekani mkazi wa jimbo la Michigan, Lione Lionel Rayford, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kukutwa na zaidi ya kilo mbili dawa za kulevya.
Mmarekani huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria Namba 15 (1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sheria Namba 15 ya mwaka 2017. Inayosomeka pamoja na paragrafu 23 ya Jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 marejeo ya 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 3 ya 2016.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Constantine Kakula amedai kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 4, 2018 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Wanjah Hamza inedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa alikutwa akisafirisha Madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye uzito wa kilogramu 2.188.
Hata Hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Madawa ya kulevya hadi mahakama Kuu au mpaka wapate kibali kutoka kwa DPP.
Kufuatia hayo, mahakama imeamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi Julai 19, 2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Hivyo makala MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA
yaani makala yote MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mmarekani-kizimbani-kwa-kukutwa-na-kilo.html
0 Response to "MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA"
Post a Comment