title : MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA
kiungo : MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA
MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 3 Mwaka huu inatarajia kuwasomea maelezo ya awali, (PH) viongozi wa Klabu ya Simba, akiwemo Rais wake Evans Aveva na Makamu wake ambao wanakabiliwa na kesi ya kughushi na kutakatisha fedha.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba ameeleza hayo leo ambapo kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro ameiomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine ya kuja kuwasomea washtakiwa hao PH.
Aidha Kimaro ameieleza Mahakama hiyo kuwa kuanzia sasa, kesi hiyo itakuwa ikiendeshwa na maofisa kutoka ofisi ya DPP wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru).Wakili Nehemia Nkoko na Nestory Wandiba, waliutaka upande wa kuharakisha kuwasomea maelezo ya awali wateja wao kwa sababu wanaendelea kuteseka mahabusu.
Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya (PH).Washtakiwa wengine ni Zacharia Hanspoppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba na mfanyabiashara, Franklin Lauwo, ambao mpaka sasa bado hawajakamatwa.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo kughushi ambapo inadaiwa kati ya Machi 10 na 16 mwka 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.
Hivyo makala MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA
yaani makala yote MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mahakama-yataja-tarehe-ya-kuwasomea.html
0 Response to "MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA"
Post a Comment