title : TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA
kiungo : TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA
TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati chini akifuatilia takwimu zinazotolewa na mfumo wa ufatiliaji wa magonjwa nchini pamoja na wadau wa Kituo cha Kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) wakati wa kikao kuhusu hali ya utekelezaji katika kufuatilia, kutoa taarifa na kudhibiti magonjwa nchini.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wadau wa Kituo cha Kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) kuhusu hali ya utekelezaji katika kufuatilia, kutoa taarifa na kudhibiti magonjwa nchini.
MWAMBA WA HABARI
Tanzania imepata pongezi kutoka kwa Kituo cha Kimataifa cha kufuatilia , kutathimini , kutoa taarifa na kuchukua hatua (CDC) kwa kufanya vizuri katika utekelezaji huo hasa katika magonjwa ya mlipuko.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa kikao cha kuangalia hali ya utendaji katika sekta ya Afya nchini.
"Wenzetu wa CDC kutoka Marekani wanatusaidia kujenga uwezo wa kufuatilia , kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa ya mlipuko kama vile Ebora na Kipindupindu na wameridhika kwa utendaji wetu hapa nchini" alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imeimarika katika kufanya uchunguzi , kutathimini , kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa mbalimbali.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa magonjwa hayana mipaka hivyo ni lazima kuwa waangalifu na kuchukua hatua mda wote kwa kujenga mifumo imara ya ufuatiliaji.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi. Inmi Petterson amesema kuwa wamefurahishwa na kazi ya wataalamu wa afya waliowekwa hapa nchini katika kupambana na magonjwa na kuahidi kuongeza nguvu kubwa ikiwemo vitendea kazi.
Aidha Balozi Inmi amesesema kuwa Serikali ya Tanzania inatakiwa kushirikiana na wananchi wa Tanzania katika kupata taarifa sahihi za magonjwa na kujenga nchi yenye wananchi wenye afya bora.
Hivyo makala TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA
yaani makala yote TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tanzania-yapongezwa-utoaji-taarifa.html
0 Response to "TANZANIA YAPONGEZWA UTOAJI TAARIFA MAGONJWA KIMATAIFA"
Post a Comment