title : HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA
kiungo : HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA
HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA
Na Woinde Shizza,Arusha
OFISA Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwalimu Sara Kibwana amesema halmashauri hiyo imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla ngazi ya Mkoa kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyofanyika Juni 6 mwaka huu.
Akizungumza leo wilayani hapa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imezawadiwa vikombe vitano kutokana na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana na mpira wa wavu wasichana.Ameongeza pia mpira wa mikono wasichana na mpira wa kengele pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.
Kibwana amesema siri ya ushindi huo ni pamoja na maandalizi mazuri yaliyofanyika kwani halmashauri hiyo ilitoa maelekezo zaidi ya miezi 9 iliyopita kwa walimu wakuu wa shule za msingi.Ambapo yalilenga kuhakikisha kila wiki wanafunzi wanakua na siku za kufanya michezo.Pia maandalizi yalikuwa mazuri wakati wa michezo kwani wachezaji walijiandaa kikamilifu kwa kukaa siku tano kambini.
Wakati huo huo Ofisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Senyaeli Pallangyo amesema uchaguzi wa wachezaji umefanyika kwa kuzingatia viwango vilivyofanyika kuanzia ngazi ya chini hadi Wilaya."Ushindi huo mkubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa makocha sambamba na wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kufuata taratibu za michezo,"amesema .
Jumla ya wachezaji 25 kutoka timu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Meru na makocha wanne wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Arusha .Imeelezwa kuwa ikumbukwe Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka huu imekuwa mshindi wa kwanza na wa jumla kwa ngazi ya Mkoa wa Arusha wenye Halmashauri 7.
Picha ni vikombe ambavyo halmashauri ya meru imevishinda (picha na Woinde Shizza,Arusha0.
Hivyo makala HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA
yaani makala yote HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/halmashauri-ya-meru-yashika-nafasi-ya.html
0 Response to "HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA"
Post a Comment