Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM

Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM
kiungo : Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM

soma pia


Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM

NA SULEIMAN MSUYA, KILOSA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imetenga Sh. milioni 46 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (CBFM) katika vijiji vitatu.

Hayo yamesemwa Mkuu wa Idara ya Maliasili, Ardhi na Misitu wilaya ya Kilosa, Ibrahim Ndembo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapo .Ndembo alisema halmashauri imekubali kutenga fedha hizo ili kuweza kuendeleza jitihada ambazo zimefanywa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) katika vijiji 20 vya wilayani hapo.

Alisema halmashauri katika kutekeleza dhana ya CBFM iliyoanza kutekelezwa na Mradi wa TTCS wataanz katika vijiji vitatu ambavyo ni New Mamboya, Inyunywe na Nyangala kata ya Mamboya."Zipo taarifa kuwa hawa ndugu zetu wa TTCS ambao wanatekeleza dhana ya CBFM katika vijiji 20 wanatarajia kuondoka Novemba mwaka hivyo ili kuendeleza lengo lao halmashauri imetenga Sh.Mil 46 ambayo itatumika kwenye vijiji vitatu vya maeneo ya Kaskazini mwa Kilosa," alisema.

Alisema CBFM kuanzishwa katika vijiji hivyo vya New Mamboya, Inyunywe na Nyangala itasaidia kuokoa misitu ambayo inaharibiwa kwa wingi.Mkuu huyo wa idara alisema lengo lao lilikuwa ni kutekeleza dhana ya CBFM katika vijiji vitano kila mwaka wa fedha ila kutokana na uhaba wa fedha wataanza na vijiji hivyo vitatu.

Ndembo alisema matarajio yao ni kupitia Baraza la Madiwani katika mwaka wa fedha 2019/2020 watatenga fedha nyingine kwa ajili vijiji vingine vya Kaskazini hasa Dumila ili kufikia vijiji 20 mwaka 2021.Mkuu huyo wa idara alisema Kilosa ina vijiji 139 na vijiji ambavyo vinatekeleza CBFM ni 20 na vyote vipo Kusini. KUSOMA ZAIDI BONFYA HAPA>>>>>>

Kaimu Meneja Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), ambaye ni Ofisa Kujenga Uwezo wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Simon Lugazo akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Kilosa kuhusu mradi wa TTCS kufikia mwisho 2019. (Picha na Suleiman Msuya).



Hivyo makala Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM

yaani makala yote Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kilosa-yatenga-shmilioni-46-za-cbfm.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM"

Post a Comment