KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI
kiungo : KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI

soma pia


KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akifafanua jambo kwa wahandisi washauri (hawapo pichani) wakati wa kongamano la wahandisi hao la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.
 Baadhi ya wahandisi washauri wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi  Dkt. Leonard Chamuriho  (hayupo pichani) wakati wa kongamano la wahandisi hao la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.
Baadhi ya wahandisi washauri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Dkt. Leonard  Chamuriho wakati wa kongamano la wahandisi hao la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.
Picha na MAELEZO
..........................................................................
Na Grace Semfuko
Maelezo

 KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi  na Mawasiliano  anayeshughulikia Uchukuzi Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema kuwa ipo haja kwa Wahandisi washauri nchini kuunda taasisi ya pamoja ya ushauri ili kuinua  taaluma hiyo, ambayo itafanya kazi kwa ufanisi kwenye sekta ya ujenzi.

Chamuriho amesema,”Iidadi ya taasisi za uhandisi ushauri zilizosajiliwa nchini ni 413, zenye wahandisi wa ndani 213 ikiwa ni sawa na wastani wa wahandisi 2 kila taasisi moja hatua ambayo inatajwa kutokuwa na ufanisi wa kizalendo wa usimamizi wa miradi ya ndani”
Amesema hayo wakati akifungua kongamano la siku moja la Wahandisi washauri wa ndani lililoandaliwa na Bodi ya Ushauri wa Wahandisi- ERBna kuongeza kuwa, iwapo wahandisi washauri watakuwa na taasisi ya pamoja itasaidia kuleta ufanisi wa miradi itakayosimamiwa na taasisi hiyo ambayo  ni ile iliyojengwa kwa weledi mkubwa.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya ERB Mhandisi Profesa Ninatubu Lema amewataka wadau wa sekta ya uUenzi nchini kutumia wahandisi washauri wa ndani, kwani wamekuwa wakifanya kazi za ushauri wa miradi mikubwa.Miradi hiyo ni kama  ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge,ujenzi wa barabara za juu za kupishana Fly Overs,majengo makubwa ya kisasa pamoja na miradi mingine.
“Kuna watu wanadhani tunawategemea sana Wahandisi wa Kigeni,Hapana! Watanzania tunaweza,ndugu zangu tuwatumie wahandisi washauri wa ndani kwani wanaweza kufanya makubwa,majengo mengi makubwa ya hapa nchini yamejengwa na yanaendeiea kujemgwa na Wahandisi wa ndani,tuwaamini,tuwape kazi” amesema Profesa Lema.
Akisisitiza jambo hilo,Profesa Lema amesema kuwa  kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na ERB hivi sasa imerahisisha  kutoka eneo moja kwenda lingine. Hii imetokana na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , yenye usimamizi madhubuti wa Rais  Dkt. John Pombe Magufuli  na kuwa na miundombinu mizuri ya barabara , ambapo zamani ilikuwa vigumu kuifikia Tanzania yote kwa muda mfupi.
Akifafanua kuhusu kongamano hilo  Lema amesema, kuwa kongamano hilo la Wahandisi washauri linafanyika Jijini Dar Es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa ERB.  Bodi hiyo ya ushauri wa wahandisi  ilianzishwa na Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania Oktoba 10 mwaka 1968 na mpaka sasa imeshafanya ushauri wa miradi mingi nchini.
Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandishi ERB Mhandisi Patrick Barozi amesema ili kukidhi Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda,wahandisi wanahitaji kufanya kazi kwa uzalendo zaidi.

Bodi hiyo ya Wahandisi ina jumla ya wahandisi waliosajiliwa 22226 elfu kati ya hao wahandisi Wanawake ni 2200 ambao ni sawa ya asilimia 9.9 ya waandisi wote . Aidha wahandisi washauri ni  413 


Hivyo makala KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI

yaani makala yote KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/katibu-mkuu-wizara-ya-ujenzi-awataka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI"

Post a Comment