JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA

JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA
kiungo : JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA

soma pia


JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amewaagiza wataalam wa sekta ya afya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kutunza vifaa tiba vilivyotolewa kwa msaada kutoka Taasisi ya Dhi Nurein Foundation.

Taasisi hiyo imesaidia ujenzi wa jengo la dharula, wodi ya wazazi, pamoja na vifaa mbalimbali vya afya ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Sh.Milioni 900. Hatua hiyo ya taasisi hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine hapa nchini. 

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Jafo amesema taasisi hiyo inaungana na taasisi zingine hapa nchini zinazosaidia miradi mbalimbali na kuagiza vifaa hivyo kulindwa na kutunzwa bila kupoteza. 

Jafo amesema kuna baadhi ya watu wachache hapa nchini wasio waadilifu wamekuwa na tabia ya kuchukua vifaa vizuri vya hospitali na kuvihamishia katika hospitali zao binafsi. Wakati huo huo, Waziri Jafo amewapongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, pamoja na Mbunge wa Bagamoyo Shukuru Kawambwa kwa kufanikisha upatikanaji wa mradi huo.

Pia Jafo amewaomba wananchi wajiunge katika mifuko mbalimbali ya bima ya afya ikiwemu CHF iliyo boreshwa ili waweze kupata huduma bora ya matibabu wao na familia zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Bagamoyo
Dkt. Saleh kutoka nchini Saudia kutoka taasisi iliyofadhili mradi huo akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo.
Wananchi wa Bagamoyo wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa afya ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja mjini Bagamoyo.


Hivyo makala JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA

yaani makala yote JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/jafo-awaagiza-wataalam-bagamoyo-kutunza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA"

Post a Comment