title : Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini
kiungo : Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini
Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake vijijini y kukagua miradi ya umeme REA III inayoendelea huku akilazimika kuzindua umeme usiku.
Amesema amelazimika kufanya uzinduzi huo usiku ili kutoa maana halisi ya uwepo wa mwanga wa umeme kwa wananchi ili nao waone hali halisi kuliko ya jinsi raha ya umeme ilivyo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato, alisema kuwa Serikali pamoja na watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kushirikiana na REA wamekuwa wakifanyakazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi ya uunganishaji umeme inafanyika kwa maslahi ya wananchi na kuvutia wawekezaji hasa wa viwanda.
“Ninawashukuru sana wananchi kwani watu wengi wana shauku ya umeme na kila unapokwenda ukiwaambia leo ninakuja kuwaunganishia umeme wako tayar kusubiri mpaka usiku, niwapongeze wananchi kwa kweli walikuwa na shauku kubwa na leo wamepata furaha.
“Na mimi kama mbunge wao bahati nzuri ni Waziri wa Nishati ilikuwa ni lazima kuwatembelea hata kama ingekuwa usiku. Lakini pia huu ni mwanga ili udhibitishe kama ni mwanga ni vizuri ukawasha usiku ikaonekana kuwa kweli hii ni taa. Nadhani walitaka wajiridhishe na wameshuhudia kwa sababu tumewasha usiku na kwangu nitatembea usiku na mchana kuwatumikia Watanzania ili mradi nitahakikisha wanapata maendeleo,” alisea Dk. Kalemani
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme
Wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato, wakimsikiliza kwa Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani
Diwani wa Viti Maalumu, Grace Kubilima (CCM), ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Ihanga, akimshukuru Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, baada ya kuzindua umeme jana usiku katika kijiji hicho.

Hivyo makala Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini
yaani makala yote Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/dk-kalemani-azindua-umeme-usiku-vijijini.html
0 Response to "Dk. Kalemani azindua umeme usiku vijijini"
Post a Comment