title : CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI
kiungo : CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI
CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Mawenzi ilipo Moshi Mjini huku kikitumia nafasi hiyo kuahidi kuenddelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa kampeni hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.
Polepole amewaomba wananchi wa Kata ya Mawenzi kumpatia kura za ushindi mgombea wa CCM Apaikunda Ayo Naburi kuwa Diwani wa Kata hiyo ili awe kiungo cha fursa zitokanazo na Serikali ya CCM kwa wananchi wake.
Akifafanua kuhusu fursa hizo za wananchi Polepole amesema CCM imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata mikopo ya Halmashauri bila usumbufu, mizengwe wala riba.
Pia wafanyabiashara wadogo wadogo waendelee kufanya shughuli zao kwa utaratibu mzuri pasina usumbufu na Vijana wa bodaboda na bajaji watazamwe katika jicho la utu, usawa na haki katika shughuli zao za usafirishaji wa abiria katikati ya mji wa Moshi.
"Naomba mtupatie Apaikunda awe jicho letu, mtu tunaye muamini, ndio kiungo akisema nasi tunatoa maelekezo kwa manufaa ya wananchi," amesema Polepole.
Uzinduzi huo wa kampeni, ni muendelezo wa mikutano ya kampeni ya uchaguzi Mdogo katika kata na majimbo ambapo CCM inaendelea kunadi Sera zake bora kwa wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akiwahutubia Wananchi na wafuasi wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,
amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.
Hivyo makala CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI
yaani makala yote CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/ccm-yazindua-kampeni-kata-ya-mawenzi.html
0 Response to "CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI"
Post a Comment