title : BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO
kiungo : BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO
BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Michuano ya Kagame Cup 2018 yanafikia kilele chake siku ya kesho tarehe 13 Julai kwa kuzikutanisha Azam na Simba katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Nicolaus Musonye amesema timu mbili kutoka Tanzania ambazo ni Simba na Azam zimefanikiwa kuingia fainali na zitakutana kesho ili kumfahamu Bingwa mpya wa michuano hiyo kwa mwaka 2018.
"timu zilizofanikiwa kutinga fainali ni Azam pamoja na Simba na mchezo huo utachezwa kuanzia majira ya saa 12 jioni katika Uwanja wa Taifa,"amesema Musonye
Mchuano huo utafanyika majira ya saa 12 jioni ,huku akiwapongeza wadau wote wa mpira Kwa kutoa michango yao kwa Hali na mali mpaka hapo walipofikia .
Musonye ameeleza kuwa timu 12 zote zilizoshiriki Kagame Cup zimefanya vizuri kwenye mashindano hayo na wajitahidi, kwenye mashindano yajayo wasivunjike moyo Kwa wale wasiofanikiwa kuingia fainali.
Sanjari na hilo, Musonye amesema amepokea maombi kutoka nchi zingine za jirani kujiunga kwenye michuano hiyo ikiwamo Zambia,malawi pamoja na Congo .
Musonye amewaomba Wadau na mashabiki wa timu hizo wajitokeze Kwa wingi na viingilio vitakuwa vya bei ya kawaida ili watu wote waweze kumudu kuingia japo mpaka sasa havijatangazwa rasmi alisema Musonye.
Hivyo makala BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO
yaani makala yote BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/bingwa-wa-kagame-cup-kujulikana-kesho.html
0 Response to "BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO"
Post a Comment