title : Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar.
kiungo : Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar.
Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar.
Na.Kijakazi.Abdalla.
Wizara ya Biashara na Viwanda na masoko Zanzibar inatarajia kuzindua mfumo wa Usajili wa Biashara na amana kwa mali zinazohamishika kutumia mtandao wa komyuta.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Migombani Zanzibar Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Amina Salum Ali amesema kuwa mfumo huo wa usajili wa kutumia mtandao ni miongoni mwa matokeo ya jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za kuhakikisha taratibu za uanzishaji na uendeshaji wa biashara Zanzibar unaimarika.
Alisema kuwa lengo la mfumo huo wa usajili biashara ni kurahisisha urasimishaji na uendeshaji wa biashara Zanzibar, kuwapunguzia gharama na muda wafanyabiashar na kupelekea kuvutiwa wawekezaji nchini .
Aidha Mhe, Amina alisema kuwa mfumo huo mpya utakuwa na faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondokana na usumbufu nakupelekea kuimarika upatikanaji wa huduma za usajili.
Pia alisema kuwa mpango huo utaimarisha utunzaji wa kumbukumbu na upatikanaji wa taarifa za wateja pindi pale zinapohitajika.
Hata hivyo alisema kuwa mfumo huo wa usajili wa biashara utaimarisha mashirikiano miongoni mwa taasisi za kodi nazile taasisi nyengine zinazohusika na uanzishaji biashara kwakuwepo kituo kimoja cha usajili.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 25/06/2018 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT,ALI Muhamed Shein ambae anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil kikwajuni Mjini Unguja .
Hivyo makala Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar.
yaani makala yote Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wizara-ya-biashara-na-viwanda-zanzibar.html
0 Response to "Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar."
Post a Comment