title : WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI
kiungo : WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI
WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu (Mb), amefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kukagua utoaji wa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri alifahamishwa kwamba mashine zote za tiba ya mionzi ya nje inafanya kazi vizuri na huduma zinaendelea kutolewa kwa wagonjwa.Pia wakati wa ziara hiyo, Mhe.Ummy alitumia fursa hiyo kuzungumza na wagonjwa mbalimbali waliokuwa wakipata huduma za tiba ya mionzi hospitalini hapo, huku baadhi ya wagonjwa walitoa malalamiko kwa Waziri kuwa, wamekuwa wakitumia muda mrefu kusubiri kupata huduma hususani huduma za mionzi ya nje.
Kufuatia hali hiyo, mhe. Ummy alitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ambao utapunguza muda kwa wagonjwa kusubiri huduma za mionzi ikiwemo kuwepo na ratiba ambayo kila mgonjwa atajua anafika saa ngapi kupata tiba hiyo.
Vile vile, mhe. Ummy alitembelea kitengo cha utoaji wa huduma za mionzi ya ndani ambapo alijionea changamoto ya kutokufanya kazi kwa mashine hizo za utoaji wa mionzi ya ndani kutokana na kukosekana kwa vifaa vya 'transfer tubes' na 'gyn applicators'.
Kufuatia hali hiyo mhe.Ummy alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage kuhakikisha kuwa mashine hizo zinafanya ndani ya siku 2 kwa kuazima hivyo vifaa hivyo kutoka Hospitali ya Bugando ili kurudisha huduma hizo kwa wagonjwa ambao wengi ni wanawake wenye tatizo la Saratani ya Mlango wa Kizazi.
"Naelekeza kuwa fanyeni utaratibu wa kupata kifaa kilichoharibika mapema iwezekanavyo" alisema mhe.Ummy.Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , Dkt.Julius Mwaiselage alimhakikishia mhe.Waziri kuwa atajitahidi ili vifaa vilivyoharibika vinapatikana ndani ya siku mbili kutoka Hospitali Bugando na pia wameagiza vifaa hvyo kutoka kiwandani nje ya nchi kwa gharama ya Euro 43,200.00
Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu juu ya ufanisi wa mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza malalamiko ya mama aliekuwa akisubiri matibabu ya ugonjwa wa kansa katika taasisi hiyo ya Ocean Road. Wa katikati ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsililiza ndugu wa moja kati ya wagonjwa waliofika Hospitalini hapo kupata huduma za matibabu ya Saratani.
Hivyo makala WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI
yaani makala yote WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/waziri-ummy-atembelea-taasisi-ya.html
0 Response to "WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI"
Post a Comment