Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao
kiungo : Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

soma pia


Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, AnnMary Mugo akinena jambo.

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kuzikatia bima nyumba zao ili wanufaike na fidia pindi nyumba hizo zikipatwa na majanga ya aina mbalimbali kama vile kuungua, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, Maryanne Mugo wakati akizungumzia bima ya nyumba itolewayo na kampuni hiyo.

Alisema, jamii inatakiwa kuwa na mwamko katika kujiunga na bima hiyo ambapo malipo yake sio makubwa ikilinganishwa hasara inayoweza kutokea pindi nyumba ikikutwa na majanga mbalimbali.

Alisema,“ jamii inapaswa kutambua kuwa kuna amani na faida kubwa iwapo wakizikatia bima nyumba zao na hiyo inajidhihirisha pindi pale ambapo nyumba zikipatwa majanga iwe kuungua moto, kuvunjwa, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale huwa bima inalipa”

Akizungumzia kuhusiana na mwamko wa watu kutumia huduma ya bima ya kampuni hiyo, alisema mpaka sasa wanao wateja 210 ambapo kati yao ni wawili tu ndo wamepatwa na majanga, mmoja ameshalipwa na mwingine anakaribia kulipwa.

Aliongeza, kuwa kuna dhana kati ya watu mbalimbali wakifikiria kuwa inachukua muda mrefu sana tangia nyumba ikipatwa majanga na kulipwa fidia ambapo alisema kwa kampuni hiyo huchukua muda mchache tu iwapo taratibu za malipo zikishakamilishwa.

Alisema, mteja hulipwa iwapo tu atakamilisha nakala muhimu kama vile ripoti ya Polisi, Makadirio ya vitu vilivyopotea au kuharibiwa ambavyo vinatokana na ripoti ya mpimaji au mkadiriaji wa bima.

“Hivi ni vitu muhimu na vya haraka vinavyotakiwa kuwakilishwa na mteja pindi nyumba yake itakapopatwa na majanga ya aina yoyote ile na kampuni za bima zinashughulikia kwa wakati”alisema.


Hivyo makala Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

yaani makala yote Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/watanzania-watakiwa-kuzikatia-bima.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao"

Post a Comment