title : WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI
kiungo : WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI
WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI
*Kamanda wa Polisi Kigoma aelezea hatua kwa hatua namna ilivyotokea
Na Ripota Wetu, Kigoma
WATU 10 wamefariki dunia na wengine 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Tabora kuligonga treni.
Akizungumzia ajali hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martine Otieno amesema imetokea eneo la kivuko Bungo Relini mkoani humo.Amefafanua dereva wa basi licha ya kupigiwa honi na treni hakusimama eneo la kivuko na hivyo akagongwa.
Ameongeza baada ya kutokea ajali hiyo abiri 10 wamepoteza maisha wakiwamo saba waliofariki eneo la tukio na wengine watatu walifariki dunia wakiwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda Otieno amesema ndani ya basi kulikuwa na jumla ya abiria 18 pamoja na dereva na utingo wake na kufanya jumla ya idadi waliokuwamo kufikia 20.Ameeleza kiss kati ya hao waliofariki dunia wanaume ni saba na wanawake watatu.
Pia amesema baada ya basi holiday kugonga treni liliburuzwa umbali wa mitambo 100 na hivyo kusababisha majeruhi wengine 17 waliokuwamo pembezoni mwa reli. "Katika ajali hiyo waliokuwamo ndani ya basi ni watu 20,waliopoteza maisha ni 10,maheruhi tisa na mmoja amenusurika na majeruhi wengine 17 hawa waliokuwamo pembezoni mwa reli.
"Hivyo idadi ya majeruhi wote ni 26 na chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliamini atawahi kuvuka kivuko cha reli na matokeo yake amesababisha kutokea kwa ajali hiyo, "amesema Kamanda Otieno.
Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa kigoma.
Hivyo makala WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI
yaani makala yote WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/watu-10-wafariki-dunia-kigoma-baada-ya.html
0 Response to "WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI"
Post a Comment