title : VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA
kiungo : VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA
VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
KATIKA kuadhimisha miaka kumi ya M-PESA kampuni ya simu ya mkononi Vodacom Tanzania imesherekea hafla hiyo ya kwa kutoa futari kwa wateja wake na kuwahamasisha waendelee kutumia huduma hiyo ya haraka na uaminifu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika Mlimani City jijini Dae es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula, amesema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega, kusimamia fedha za wateja na kuhakikisha hakuna wizi au utapeli kupitia mitandaoni.
Pia amewapongeza Vodacom kwa kuwa kinara wa wateja wengi wanaofanya miamala ambapo kwa mwezi Machi tu wateja zaidi ya milioni nane walifanya miamala ya kifedha.
Nae Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao amesema sherehe hizo zitaendelea kufanyika katika mikoa tofauti nchi nzima kwa kuwa huduma M-PESA ndiyo inayoongoza nchini Tanzania ikiwa imekamata asilimia 42 ya soko, watumiaji hai zaidi ya milioni 8.2.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula ( wa sita kushoto) akiiongoza meza kuu kushuhudia magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa yaliyotolewa wakati wa hafla ya kutimiza miaka kumi ya M-Pesa iliyofanyika jana Jijini Dsm. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema (wa tano kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary na Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi.
Mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 10 ya M-Pesa, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, wakifuatilia moja ya burudani wakati wa sherehe ya kusherehekea mika 10 ya M-PESA iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (katikati) wakati wa hafla ya kusherekea miaka 10 ya M-pesa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Ian Ferrao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia akimsikiliza mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mary Majula wakati wa hafla ya kusherekea miaka 10 ya M-pesa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (kulia) akisalimiana na balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thomsanga Msekelu wakati wa Sherehe ya Kusherehekea miaka 10 ya M-pesa iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Moja ya magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa yakiwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuzinduliwa wakati wa sherehe kusherehekea miaka 10 ya M-pesa .Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa M-Pesa, Polycarp Ndekana na mshereheshaji Taji Liundi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary (katikati) na Mkuu wa kitengo cha Mwendelezo wa Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya gari kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-pesa wakati wa sherehe ya kusherehekea miaka k10 ya M-pesa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA
yaani makala yote VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/vodacom-yasherekea-miaka-10-ya-m-pesa.html
0 Response to "VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA"
Post a Comment