title : MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA
kiungo : MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA
MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema magari ya Serikali ndio yanayoongoza kuvunja sheria kwa kupita kwenye barabara ya mabasi ya mwendo kasi na hivyo limesema ni marufuku gari hayo kupita kweye baabara hiyo.
Kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo jeshi hilo limesema litaanza kufanya operesheni maalum kukomesha hali hiyo na kwamba dereva ambaye atakamatwa atachukuliwa hatua.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ambapo amefafanua kumwekuwa na tabia ambayo sasa inaota mizizi ya madereva kuhama kwenye barabara inayohusika na kuingia barabara ya mabasi ya mwendo kasi.
"Vyombo vya ulinzi madereva wake wengi wanapita katika barabra hiyo,magari ya wagonjwa nayo wakati yanapeleka mgonjwa na hata wakati wa kurudi pamoja na dereva kuwa peke yake bado anapita katika barabara hiyo. Matokeo yake inakuwa vurugu kwani ni matumizi ambayo hayakukusudiwa"amefafanua.
Hivyo Kamanda Mambosasa ametoa rai na onyo kwamba ni vema barabara zikatumika kwa mujibu wa sheria na hakuna sababu ya kulazimisha kubadilisha matumizi ya barabara hiyo ya mwendo kasi.
"Juzi Ambulance imesababisha mauaji au vifo vya wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na uzembe ulifanywa na dereva wa Ambulance hiyo kwa kulazimisha kupita katika barabara ambayo hakuwa anaruhusiwa na matokeo yake akawa anapambana na magari yanayokuja mbele yake.
"Katika kulazimisha kupita akaligonga gari iliyokuwa imesimama na matokeo yake akasababisha ajali hiyo ambayo imepoteza maisha ya wanafunzi hao."Hatuwezi kuacha hali hii ikaendelea kuota mizizi, hivyo tutafanya operesheni na dereva ambaye tutamkamata asipige mayoe .Magari ya Serikali yanaoongoza kwa kuvunja sheria na kupita kwenye barabara za mwendo kasi,"amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza operesheni hiyo inaanza leo kwa kuwachukulia hatua wote wanaovunja sheria na kwamba matokeo yake yataonekana.
Wakati huohuo Kamanda Mambosasa amepiga marufuku mchezo wa kuvaa viatu vya matairi na kisha kukimbia barabarani huku magari yakipita kwa kasi na kwamba wanaofanya mchezo huo waache mara moja kwani polisi itawakamata na kuwachukulia hatua.
Amesema kila mchezo una maeneo yake ya kuchezea hivyo hakuna sababu ya barabara za Serikali kutumika kwa mchezo huo na ole wao watakaokamatwa.
Hivyo makala MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA
yaani makala yote MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/magari-ya-serikali-ndio-yanayoongoza.html
0 Response to "MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA"
Post a Comment