RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU

RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU
kiungo : RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU

soma pia


RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU


WATENDAJI wa ngazi mbalimbali Mkoani Tabora wameagiza kuanza zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu ambao wamekuwa na tabia ya kuchoma moto ovyo wakati wa maandalizi ya mashamba na wengine kwa ajili ya kutaka nyasi ziote upya kwa ajili ya mifugo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey MwanriMwanri alitoa kauli hiyo jana Wilayani Uyui wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Kakola na Msimba akiwa katika kampeni ya kuhimiza wananchi kujiunga na Ushirika na kupinga vita utoro na mimba za utotoni.

Alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya watu kuanza kuchoma ovyo moto ambao umekuwa ukisababisha hasara kubwa katika mistu na hata kuunguza miti iliyopandwa hivi karibuni.

Mwanri alisema kuanza ni marufuku kuandaa mashamba yao kwa kuchoma moto kwani wamekuwa wakiuacha na kusambaa maeneo mengine na hivyo kuleta athari katika mistu ya asili na viumbe wengine.

Aliwataka wananchi na wakulima mkoani humo kuandaa mashamba kwa njia ya kisasa bila kuathiri mazingira pamoja na viumbe hai wengine hatua ambayo itawezesha kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Katika kukabiliana na tabia hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo  amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kwamba wanawachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kufanya uharibifu huo kwa kuwa haiwezekani mtu akachoma moto asijulikane .

Alisema katika kijiji au Kata ambayo atakuta watu wamechoma moto na umeteketeza miti iwe ya kupanda au asili kiongozi huyo atawajibika kwa kushindwa kusimamia sheria.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa misitu mingi ya asili na miti mingi iliyopandwa katika kipindi cha mvua za masika ipo hatarini kutokana na baadhi ya watu ambao wameanza kuchoma ovyo mistu. 

Alitaja sababu  kubwa ya uchomaji moto huu wengine ni kwa sababu ya uvivu wa kuandaa mashamba yao  kwa kupalilia na wengine kuadai kuwa wanapochoma moto wanapata malisho mapya ya mifugo jambo ambao sio rafiki kwa mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwahotubia wakazi wa Kijiji cha Msimba wilayani Uyui wakati akiwa anendelea na kampeni jana katika vijiji mbalimbali ya kusisitiza vita dhidi ya  utoro na mimba za utotoni na uchomaji moto ovyo mistu mkoani humo.Picha na Tiganya Vincent



Hivyo makala RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU

yaani makala yote RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/rc-tabora-kupambana-na-wachomaji-moto.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU"

Post a Comment