MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI

MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI
kiungo : MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI

soma pia


MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI

Na Frankius Cleophace Serengeti

SHIRIKA la Righ to Play linaendelea na matamasha katika kata za  wilayani Serengeti mkoani Mara kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na masuala ya ukatili wa ijinsia dhidi ya watoto.

Elimu hiyo inayotolewa inazungumzia kupiga vita ukeketaji kwa mtoto wa Kike, mimba za utotoni, vipigo kwa watoto, kuchomwa moto pamoja na kuhakikisha wanapata haki ya elimu bila kubagua jinsia.

Akizungumzia kuhusu tamasha lililofanyika kata ya Uwanja wa Ndege, Leah Kimaro kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY amesema  lengo la Shirika ni kuhakikisha wanabadili mitazamo ya jamii ili kuondokana na mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati ili kumkomboa mtoto wa kike ambaye kwa Serengeti amekuwa akiachwa nyuma kutokana na mila hizo.

Ofisa Maendeleo Jamii Kata ya Uwanja wa Ndege Josepha Dismas ameitaka jamii kuendelea kuthamini watoto wote bila ubaguzi wowote na kuahidi kuwa wao kama Serikali wataendelea kushirikiana na mashirika ili kuipatia jamii elimu iliyokusudiwa.

“Hii elimu inayotolewa kupitia michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu kwa wasichana jamii inazidi kuamini kuwa Mtoto wa kike anaweza bila kuwezeshwa."Hivyo sasa ni jukumu letu kama viongozi ngazi za jamii kushiriki kikamilifu na kuzidi kulaani Vikali ukatili unaofanyika kwa Watoto,” amesema Josepha.

Pia Ofisa Maendeleo ameongeza kuwa michezo hiyo imezidi kukusanya watoto wengi na maudhurio kuongezeka mashuleni,hivyo wazazi wameombwa kuruhusu watoto wao ili washiriki michezo.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege  Josepha  Dismas akikabidhi Kapteni wa Timu ya  Senta FC baada ya kushinda Timu ya  Burunga FC.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege  Josepha  Dismas akikabidho Kombe kapteni wa Timu ya  Vilaza Fc baada ya kushinda Timu ya Vibonde FC.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege  Josepha  Dismas akikabidhi Zawadi ya Madaftari kwa Wanafunzi hao walioshiriki Vyema katika Michezo iliyofanyika Maeneo hayo.
Wavulana wakicheza Mpira wa Pete.


Hivyo makala MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI

yaani makala yote MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/matamasha-ya-kutoa-elimu-ya-kupinga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MATAMASHA YA KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAENDELEA WILAYANI SERENGETI"

Post a Comment