title : JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU
kiungo : JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU
JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, leo Mjini Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.
“Historia ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali” ameeleza Mhe. Jafo.
Aidha amesema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.
“TAMISEMI kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko” amefafanua Mhe. Jafo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizindua Mwongozo wa Kampeni ya uanzishwaji wa Viwanda kwa kila Mkoa hapa nchini ili kuendana na dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akionesha moja ya viatu vinavyozalishwa hapa nchini katika Viwanda vidogo na vya Kati wakati akikagua mabanda ya wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za ngozi mara baada ya kuzindua kampeni yenye kauli Mbiu ya “Mkoa Wetu Viwanda vyetu” ili kuhamasisha ujenzi wa Viwanda katika Mikoa yote nchini.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa(kushoto), kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati katika kila Mkoa.
Hivyo makala JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU
yaani makala yote JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/jafo-azindua-kampeni-ya-mkoa-wetu.html
0 Response to "JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU"
Post a Comment