MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI

MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI
kiungo : MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI

soma pia


MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba wanawake wenye tabia ya kuvaa sketi fupi maarufu Vimini na nguo za kubana wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wakaacha kuzivaa katika kipindi hiki ili kuhakikisha waumini wa dini ya Kiislamu wanatekeleza funga hiyo vema.

Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anapokea msaada wa tende kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi Darul Irshad Centre Islamic Tanzania Arif Yusuf AbduRahman kwa kushirikiana na taasisi rafiki ya Muraj Islamic Centre Tanzania.Makonda ameagiza tende hizo zipelekwe katika vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Wakati anazungumzia funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo waumini wa dini ya Kiislamu wanaendelea nayo amesema ni vema waumini wa dini zote wakashiriki katika kufanikisha waliofunga wanatekeleza moja ya nguzo za dini hiyo vema.Hivyo amewaomba wanawake wenye tabia ya kuvaa vimini na nguo za kubana katika mwezi huu wakaacha kuzivaa ili kutoa nafasi ya waliofunga kutoingia majaribuni kutokana na mavazi hayo.

"Niwaombe akina dada wanaopenda kuvaa nguo za kubana hasa vimini kuacha kuvaa hadi hapo mfungo utakapokwisha.Natambua wananchi wa Mkoa wa Dar es Salam wapo wenye imani tofauti lakini bado tunayo nafasi ya kuheshimi imani ya kila mmoja wetu,"amefafanua Makonda.Pia ametoa ombi kwa wafanyabishara kutopandisha bei ya vyakula katika kipindi ambacho waumini wa dini ya Kiislamu wanaendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhan.

"Wananchi wa Dar es Salaam niendelee kutoa ombi tuwape ushirikiano ndugu zetu walioko kwenye funga na kwa wafanyabiashara msipandishe bei ya vyakula,"amesisitiza.Kuhusu tende ambazo zimetolewa na taasisi hiyo Makonda amesema zitakwenda kugawiwa vituo vya watoto yatima vilivyopo Dar es Salaam na anaamini kwa kugawa tende hizo kwenye vituo hivyo ni sehemu ya kuwakumbuka watoto walioko huko ambao wapo ambao wapo kwenye funga.
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul  Irshad  Centre Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar  es Salaam leo
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul  Irshad  Centre Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar  es Salaam leo
Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya  Darul Irshad Centre Islamic Tanzania AbduRahman leo jijini.



Hivyo makala MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI

yaani makala yote MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/makonda-awaomba-waumini-dini-zote.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKONDA AWAOMBA WAUMINI DINI ZOTE KUHESHIMU MFUNGO WA RAMADHAN, AWAGEUZIA KIBAO WAVAA VIMINI, NGUO FUPI"

Post a Comment