Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar.

Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar.
kiungo : Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar.

soma pia


Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar.

Khadija.Khamis.Maelezo.
Waziri wa Afya Mhe.Hamad Rashid Mohamed amesema Wizara yake imejipanga  kuhakikisha maradhi ya malaria yanamalizika hasa katika maeneo ambayo bado maambukizo ya ugonjwa huu yameripotiwa.
Hayo aliyasema wakati akisoma Hotuba ya  Bajeti ya Wizara ya Afya kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya mwaka 2018 hadi 2019 huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi chukwani .
Alisema katika kuhakikisha huduma za kinga zinapatikana wizara imekusudia kuhamasisha jamii juu ya usafi wa mazingira ili kujikinga na maradhi mbalimbali yakiwemo malaria,  maradhi ya kuharisha na kipindupindu .
Aidha alisema Wizara imekusudia kuhamasisha jamii juu ya masuala ya Afya kwa  kuendesha programu ya Afya maskulini pamoja na  kufuatilia mienendo ya maradhi ili kuweza kubaini mapema uwepo wa maradhi na kushukuwa tahadhari zinazostahiki.
Alifafanua wizara imekusudia kuimarisha huduma za kinga kwa maradhi mbalimbali yanayoambukiza na yasiyoambukiza na kuendeleza kudhibiti maambukizo ya maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini ( VVU).
Alifahamisha katika jitihada hizo zinatarajiwa kuimarisha  huduma za afya ya  mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga kwa kuengeza kiwango cha chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa  miaka miwili kufikia zaidi ya asilimia 90 na kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka tisa hadi 14
Waziri huyo alieleza kuwa wizara imekusudia kutekeleza mkakati  wa kitaifa wa kudhibiti maradhi unaoitwa International Health Regulation (IHR) pamoja na kuipa kipaombele kauli mbiu iliyowekwa MATIBABU BURE NI HAKI YA KILA MTU .
Aidha alisema katika kutekeleza mipango mbalimbali ya wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa matumizi ya shilling 93,253,000,000 kwa  matumizi ya kawaida, matumizi ya maendeleo na mapato  ya wizara ya afya .
MWISHO
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


Hivyo makala Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar.

yaani makala yote Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/hutuba-ya-bajeti-ya-matumizi-na-mapato.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato ya Wizara ya Afya Zanzibar."

Post a Comment