title : KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC
kiungo : KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC
KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imetangaza rasmi kuwa imemsajili kiungo Tafadzwa Kutinyu mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo huyo atachezea kikosi cha Azam FC ambacho maskani yake iko Chamazi jijini Dar es Salaam. Mchezaji huyo amekuwa na msimu mzuri tokea ajiunge na Singinda United msimu huu ambaye alitokea katika klabu ya Chicken Inn ya nchini kwao Zimbabwe.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Azam FC Jaffary Iddy amesema mchezaji huyo ambaye mkataba wake uko wazi ni mapendekezo ya mwalimu Hans Van Der Pluijm raia wa Ubolanzi.
"Tunaamini mwalimu anamfahamu vizuri ndio maana amemuhitaji.Pia tutaangalia maandeleo yake mchezaji huyo anaisaidiaje timu,akiwa anafanya vizuri basi tutamuongezea mkataba mnono zaidi" amesema na kuongeza kuwa Kutinyu atavaa rasmi uzi wa Azam katika mashindano ya CECAFA ambayo timu hiyo ndiye mtetezi wa Kombe hilo.
"Tutarejea tena kuutetea ubingwa wetu baada ya mashindano hayo kusimama kwa muda wa miaka 3 bila kufanyika"amesema Jaffary.
Hivyo makala KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC
yaani makala yote KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kutinyu-amfuata-kocha-van-der-pluijm.html
0 Response to "KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC"
Post a Comment