MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA

MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA
kiungo : MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA

soma pia


MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atashiriki bonanza lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) litakalofanyika siku ya Jumamosi tarehe 30 Juni, 2018 saa kumi na mbili na nusu asubuhi katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Bw. Moshi Makuka wakati akielezea maandalizi ya Bonanza hilo, jijini Dodoma.
Bw. Makuka amesema, bonanza hilo ni mahususi katika kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia ya kuwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda kufanya mazoezi kwa lengo la kujenga na kulinda afya zao.
Bw. Makuka amefafanua kuwa, bonanza la SHIMIWI mwaka huu ni la kipekee kwani litashirikisha Makatibu Wakuu, Watendaji Wakuu wa Serikali, Watumishi wa Umma na Wananchi wa Dodoma.
Bw. Makuka ameongeza kuwa, michezo mbalimbali itafanyika katika bonanza hilo ikijumuisha matembezi ndani ya jiji la Dodoma, mazoezi ya viungo, kukimbia, kuvuta kamba, mpira wa miguu na mpira wa pete kwa timu ambazo zimejiandaa.
Bw. Makuka ametoa wito kwa viongozi, watumishi wa umma na wananchi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo kwa faida ya afya zao.
Aidha, Bw. Makuka amesema, bonanza hilo litatanguliwa na mkutano wa viongozi wa Vilabu vya Michezo vya Wizara na Idara za Serikali utakaofanyika tarehe 29 Juni, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa HAZINA ndogo,  ili kuweka mkakati madhubuti wa namna ya kutekeleza agizo la Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
IMETOLEWA NA;

KAMATI YA HABARI NA MAWASILIANO - SHIMIWI


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/makamu-wa-rais-kushiriki-bonanza-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI JIJINI DODOMA"

Post a Comment