title : MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS
kiungo : MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS
MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forums, Micke William baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu.
Max na Micke wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona kuwa ushahidi uĺiotolewa na mashahidi hao dhidi ya washtakiwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha na kuongeza kuwa hauna mashiko.
Katika kesi hiyo namba 457 ya mwaka 2017 washtakiwa wanatuhumiwa kuwazuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi.
Kabla ya uamuzi huuo kutolewa leo, awali washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi ambae alidai Melo na William ni wamiliki na waanzilishi wa mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao umesajiliwa Brela Julai 2 mwaka 2008 na kupewa namba ya usajili 66333
Alidai baada ya usajili, hupatiwa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo wa kuona taarifa kwenye mfumo wao.
Aidha katika maelezo hayo, Kishenyi alidai Mei 10 mwaka 2016, ZCO aliwaandika barua washtakiwa akiwafahamisha ofisi yake inafanya upelelezi kuhusu taarifa ya uongo dhidi ya Cusna Investment na Ocean Link iliyochapishwa na mwanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri. ZCO pia aliwafahamisha kwa kifupi taarifa ambayo anaihitaji kutoka kwao na maelezo binafsi ya mtu aliyechapisha ili aweze kufanya upelelezi.
Alibainisha kuwa Mei 11mwaka 2016 mfanyakazi wa Jamii Media, Chrispin Mganyizi aliipokea na kuiwasilisha kwa washtakiwa lakini walikwamisha polisi kufanya upelelezi kwa kuficha taarifa za wanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri.
Kishenyi alidai kuwa kufuatia jitihada hizo za ZCO za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Hivyo makala MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS
yaani makala yote MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mahakama-yamuachia-huru-mkurugenzi.html
0 Response to "MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS"
Post a Comment