title : MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA
kiungo : MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA
MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
KAMA noma na iwe noma !Ndivyo unavyoweza kuuelezea mchezo kati ya Nigeria dhidi ya Iceland ambapo mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji machachari wa Nigeria 'Nigeria Super Eagles' Ahmed Mussa kuwafanya mashabiki wa soka Afrika kuungana na kushangalia ushindi mnono ambao wameupata.
Katika mchezo huo ambao Nigeria wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Iceland wanaotoka katika taifa ambalo idadi yake ya watu ni 350,000.Mechi imechezwa katika Uwanja wa Volgograd Arena.Kwa sasa Nigeria inajipanga kwa mchezo wake ujao dhidi ya Argentina ambayo juzi ilipoteza mchezo wake kwa kufungwa mabao matatu.
Yote kwa yote ukweli utabaki kuwa ushindi wa jana wa Nigeria ni kama vile umeifanya kikosi hicho na Bara la Afrika kuamka kutoka usingizini na kutambua nini ambacho kimewapeleka kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambayo inaendelea nchini Urusi.
Ufundi, umaridadi na matumizi ya akili nyingi yaliyotosha kuifanya Nigeria kuonekana kutawala licha ya mchezo kuwa na ushndani wa hali ya juu hasa kwa kuzingatia kikosi cha Iceland ambacho kwa sehemu kubwa wachezaji wake kuwa ni madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu hakuwa nyuma kwani walionesha soka la uhakika.
Kasi ya mchezo huo ulikuwa kibwa na takwimu za kosoka zinaelezea iwapo wangekuwa ni kukimbia basi hadi dakika ya 80 ya mchezo wachezaji walikuwa wamekimbia kilometa 47.Hivyo unaweza kupata picha ya kasi ya mchezo huo ambapo pamoja na kila aina ya ufundi kwa kila mchezaji hadi unalizika shangwe zikawaka kwa Afrika.
Unajua mshambuali wa Nigeria Ahmed Mussa kafanya nini cha ziada? Iko hivi mabao yake mawili yamesababisha kubadilsha muundo wa kundi D ambapo sasa yanaonesha Nigeria iko nafasi ya pili ikiwa na alama tatu. Katika mchezo huo kikosi cha Iceland kilipata penati dakika ya 83 lakini kiungo na mshambualiji wake Gylfi Sigurdsson alipaisha mkwaju wa penati hiyo.Hivyo hadi mchezo umalizika Nigeria 2-1.
Michuzi TV kwa kukumbusha tu kikosi cha Nigeria ambacho kimeshinda mchezo wa jana kilikuwa ni tofauti kidogo na kile kilichocheza katika mchezo wa kwanza na matokeo yakawa ni kwa Nigeria kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Croatia.
Jana wafungaji wanaoichezea Leicester City Ahmed Musa na Kelechi Iheanacho walianza kuchezwa kwa mara ya kwanza katika mechi ya kombe hilo na uwepo wao umeifanya timu yao kuonekana mahiri kwa kutawala soka.
Wakati huo huo kivuti katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Costa Rica, kivutio kilikuwa kwa mshambuliaji wa Brazil Neymar ambaye aliamua kuangalia kilio uwanjani baada ya mchezo kumalizika. Brazil iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kati ya mabao hayo ya Brazil moja limetiwa wavuni na Neymar bao lake la ufundi likaibua shangwe kwa mashabiki wa soka wa nchi hiyo. Hata hivyo kitendo cha kulia uwanjani ndicho kilioneka
na kuvutia zaidi na watu kutaka kufahamu nini ambacho kimemliza. Alipoulizwa kwanini amelia uwanjani amejibu hiyo inatokana na hisi alizonazo baada ya kuwa majeruhi kwa miezi mitatu akiwa nje ya uwanja.
Hivyo makala MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA
yaani makala yote MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mabao-ya-ahmed-mussa-yaipeleka-nigeria.html
0 Response to "MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA"
Post a Comment