title : KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE
kiungo : KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE
KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ametoa mwito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.
Kubenea ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na kuikabidhi.
Miradi aliyoitembelea Kubenea ni ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu Sh. milioni 7.7, miradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17,mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. milioni 12 pamoja na ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.
Akizungumza baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea amesema ni vyema kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama."Mimi sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya wananchi....ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea alifanya kitu fulani.
"Kwahiyo niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu Chadema...tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu," amesema Kubenea.Amefafanua kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya jospitali na shule yanahitaji kuboreshwa.
Akizungumzia miradi hiyo Kubenea amesema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.Akitoa shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mavurunza amesema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo
Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.
Hivyo makala KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE
yaani makala yote KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kubenea-awataka-viongozi-wa-kisiasa.html
0 Response to "KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE"
Post a Comment