KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO
kiungo : KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

soma pia


KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)

Wakazi wa jiji la Mwanza mapema leo wameshuhudia tukio la kushushwa kwenye maji kwa Kivuko kipya cha MV. Mwanza baada ya kufikia hatua za mwisho za kukamilika kwa ujenzi wake. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa pongezi kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kusimamia mradi huo kwa mafanikio makubwa. Aidha, ameipongeza Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza kwa kujenga kivuko hicho kwa ubora wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za vivuko kutoka TEMESA, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa TEMESA alisema ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kupata kivuko kipya kwani kitapunguza adha ya foleni ndefu kwa watumiaji wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi. 

Mhandisi King’ombe aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuhakikisha kuwa wakazi wa mkoa huo wanapata huduma ya usafiri yenye uhakika na kuwataka wakazi hao kukitunza kivuko hicho kitakapoanza kutoa huduma ya uvushaji wa abiria na magari. Alisema, hatua inayofuata baada ya kivuko hicho kushushwa kwenye maji ni ukamilishaji wa kazi chache zilizobaki na hatimaye kukifanyia majaribio ili kuhakikisha abiria na mali zao wanakuwa salama pindi watumiapo kivuko hicho.

Naye Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Alex William aliwaomba wakazi wa Mwanza kujivunia kivuko hicho kwa kuwa kimepewa jina la mkoa huo na hii ikiwa ni heshima kubwa kwa wakazi hao.Kivuko hicho cha tani 250 kina uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza hivi karibuni.
Kivuko cha MV. Mwanza kikisubiri kutoswa kwa mara ya kwanza kwenye maji kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250. Kivuko hicho kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne
Muonekano wa kivuko kipya cha MV. Mwanza mara baada ya kutoswa kwenye maji kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250 na kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne.
Muonekano wa Kivuko cha MV MWANZA mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO


Hivyo makala KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

yaani makala yote KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kivuko-kipya-cha-mv-mwanza-chashushwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO"

Post a Comment