KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA
kiungo : KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

soma pia


KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka  2006, Wema Sepetu na wafanyakazi wake hadi Juni 19 mwaka 2018.

Kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya Wema na wenzake kuanza kujitetea Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku upande wa Wakili wa Serikali Costantine Kakula na Wakili wa utetezi Albert Msendo wakiwa wapo tayari kuendelea na kesi.

Hata hivyo, Hakimu Simba anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru kikazi na kulazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Juni  19 mwaka 2018 ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.Kesi hiyo imefikia hatua hiyo baada ya Hakimu Simba kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Na kutoa uamuzi ambapo aliwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu na hivyo wanapaswa kujitetea.Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.Inadaiwa kuwa Februari 4 mwaka 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.



Hivyo makala KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

yaani makala yote KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kesi-inayomkabili-wema-sepetu-yapigwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA"

Post a Comment