title : INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE.
kiungo : INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE.
INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE.
KAMPUNI ya simu ya Infinix imeweka dhamira ya kuzalisha simu zenye teknolojia ya hali ya juu na muonekano mzuri kwajili ya kizazi kipya. Infinix NOTE 5 inaendeshwa na mfumo wa Android wenye kuifanya kuwa simu ya pekee yenye sifa zenye kushawishi ukilinganisha na simu yoyote ya Infinix kwa sasa.
Kupitia mfumo wa Android One Infinix NOTE 5 imethibitika kuwa simu yenye ulinzi zaidi wa software na inayopokea updates katika muda mfupi.
Baada ya kuzinduliwa jijini Dubai, Infinix NOTE 5 itazinduliwa katika nchi zaidi ya 30 ikiwemo Nigeria, Egypt, India, Morocco, Kenya, Uganda Cote d’ voire na nyengine nyingi.
Na katika kuhakikisha kampuni inatimiza ahadi ya kuzalisha simu zenye muonekano mzuri kuendana na wakati Infinix NOTE 5 inamuonekano wa tofauti ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 na nchi 6.0 FHD.
Pamoja ya kuwa na mfumo pendwa hasa kwa wale wenye matumizi makubwa kama ya kiofisi, lakini pia Infinix NOTE 5 imempendelea mpenzi wa kamera pia kwa kupitia pixel 16 low light selfie na pixel 12 nyuma zenye kupiga picha nzuri hata katika mwanga hafifu.
Infinix NOTE 5 inauwezo wa kukaa na chaji kwa siku tatu pasipo kuzima data kutokana na ujazo wake wa chaji kuwa 4500.
Akiongea na vyombo vya habari makamu wa raisi wa TRANSSION HOLDINGS Bwana Arif Chowdhury alisema kwamba, “nikiwa miongoni mwa wazalishaji na wasambazaji wa simu za Infinix katika masoko mbalimbali tunawahakikishia bidhaa zetu zinawafikia idadi kubwa ya watu na kuongeza utandawazi kupitia njia ya mawasiliano”.
Na mkurugenzi wa Android, Bwana Mahir Sahin alisema, “unaponunua simu mpya unategemea kuona sifa mpya katika simu hiyo na hii ndio sababu iliyotufanya tushirikiane na GOOGLE na kuwaletea simu yenye maajabu yanayotokana na Android One kupitia GOOGLE Lens na GOOGLE Assitant”.
Hivyo makala INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE.
yaani makala yote INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/infinix-imezindua-infinix-note-5-yenye.html
0 Response to "INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE."
Post a Comment