title :
kiungo :
Na.Othman Khamis OMPR.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Viongozi wa Jimbo hilo wataendelea kuwaunga mkono Wananchi wao hasa Vijana na Akina Mama walioamua kujituma katika muelekeo wa kujitafutia Maendeleo ili kujenga hatma njema ya maisha yao.
Alisema misaada ya kuyawezesha Makundi hayo katika kuyapatia vifaa, mtaji sambamba na maarifa itakuwa ikiendelea kila wakati kulingana na mahitaji halisi ya Wananchi ikilenga zaidi katika Vikundi vya Ushirika.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akikabidhi msaada wa Mashine iliyoitanguliwa na Boti ya kuvulia Samaki aliyoitoa kwa Kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Bahati Abeid Nassir kwa ajili ya Vijana wa Kikundi cha Hamasa cha Jimbo la Mahonda chenye Mastakimu yake Kijiji cha Fujoni hafla iliyofanyika Nyumbani kwake Kama Kaskazini kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema hakuna Tajiri au Kikundi cha Jamii kilichopata utajiri wa kushtukia bila ya kufanya kazi za ziada katika kujitafutia riziki ambazo Wanakikundi hao watalazimika kufanya jitihada zitakazowawezesha kujikwamua kutoka katika mazingira magumu ya maisha.
Balozi Seif aliwatahadharisha Wanachama wa Kikundi hicho cha Hamasa kwamba msaada huo wa Boti na Mshine yake usije geuka kuwa chanzo cha kuleta mifarakano baina yao.
Aliwataka Wanakikundi hao wapatao 50 walio jinsia mbili tofauti wafanye kazi kwa juhudi zao zote ili vifaa vya msaada waliopatiwa viwezeshe kuzaa vyengine kwa lengo la kutanua mradi wao unaopaswa kuwa wa kudumu.
Aliwakumbusha wana Hamasa hao kuzingatia uadilifu baina yao katika mfumo wa matumizi ya Fedha na kuepuka majungu yanayoweza kuwa chanzo cha mizozo inayoweza kuchipuka kutokana na faida itakayozalishwa.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea faraja yake kutokana na muelekeo wa Vijana walioacha dawa za kulevya wa Kijiji cha Fujoni na kupatiwa msaada wa Bot na Mashine kwa shughuli za Kiuchumi bado wanaendelea na maisha yao kwa matumaini makubwa kwenye mradi wao wa Uvuvi.
Mapema Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi alikiahidi Kikundi hicho cha Hamasa kwa upande wa Akina Mama kufikiria kuwapatia Vifaa kwa ajili ya ukaushaji wa Dagaa litalokuwa likivuliwa na Vijana wa Kiume wa Kikundi hicho.
Mama Asha alisema hatua hiyo itawajengea msingi imara utakaowawezesha kujitahidi kuwa nao ni miongoni mwa Wanakikundi hicho badala ya kusubiri kuletewa kila kitu nyumbani mfumo ambao umepitwa na wakati katika kanre ya sasa na mihangaiko ya Sayansi na Teknolojia.
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Vijana hao Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi hicho cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah alisema kitega uchumi walichopatiwa kitakuwa ni chanzo na fursa adhimu kwao itakayowasababishia kuacha tegemezi katika mazingira yao ya uwajibikaji wa kila siku.
Kichamu alisema yapo mambo yanayowakabili katika kazi zao za Kimaisha ikiwemo harakati za Kisiasa zikihitaji nguvu za uwezeshaji kifedha ambayo kwa sasa itakuwa nadra kuwafuata Viongozi wao kwa vile wameshajengewa mazingira ya kuwajibika wao binafsi.
Mashine hiyo pamoja na Boti yake vilivyotolewa na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi na Mh. Bahati Abeid Nassir vimegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 13,800,000/-.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed amewapongeza na kuwashukuru Viongozi pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo kwa kazi kubwa waliyofanya iliyowezesha kufanikisha kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 kwenye Kikao vya Baraza la Wawakilishi kinachoendelea.
Waziri Aboud kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa pongezi hizo mara baada ya Viongozi na Watendaji hao kufutari pamoja katika Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi yaliyopo Kama nje kidogo ya Kaskazini ya Mji wa Zanzibar.
Alisema Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/2019 haikuwa na vikwazo vikubwa ikilinganishwa na Bajeti zilizopita kitendo ambacho kimedhihirisha umakini na ushupavu walionao Viongozi na Watendaji hao.
Waziri Aboud alifahamisha kwamba malezi ya Kazi waliyoyapata watendaji hao kupitia kwa Viongozi wao Wakuu yamewawezesha kufanya kazi Kizalendo, wakizingatia moyo wa huruma sambamba na kupendana miongoni mwao na hatimae kupata mafanikio makubwa.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/na.html
0 Response to " "
Post a Comment