title : WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI
kiungo : WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI
WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MGANGA Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatambua umuhimu wa Mamlaka ya Maabara ya Serikali Mkemia Mkuu katika kulinda ya afya ya wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ambapo amesema kikao cha baraza ni kuhakikisha kuna kuwepo kwa uhusiano kati ya watendaji na Menejimenti.
Kambi amesema katika mkutano wa baraza wanatakiwa kujadili malengo ya taasisi na maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mafunzo ambayo yanatakiwa kutolewa kwa haki sawa.
Aidha Mganga Mkuu huyo ametaka wafanyakazi wa (GCLA) kuachana na kuwa sehemu ya watu wanaolalamika badala yake wanatakiwa kutatua changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (GCLA), Dk. Fidelice Mafumiko amesema katika kikao hicho watajadili mada mbalimbali ikiwa ni kuijenga taasisi hiyo.
Dk. Mafumiko amesema pia baraza hilo kupitia kikao hicho wataazimia mambo mbalimbali yakiwamo ya kujenga mamlaka ikiwa pamoja na masuala ya maadili.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Serikali Mkemia Mkuu (GCLA) uliofanyika katika ukumbi wa MSD jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Serikali Mkemia Mkuu (GCLA), Dk. Fidelice Mafumiko akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA kuhusiana na mada ambazo watapitia uliofanyika katika ukumbi wa MSD jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Tawi la la TUGHE wa GCLA, Juvitus Mukela akitoa neno kwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA uliofanyika katika ukumbi wa msd jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya wajumbe katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa GCLA wakifuatilia mada kwenye mkutano huo.
Picha za pamoja
Hivyo makala WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI
yaani makala yote WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wizara-ya-afya-yatambua-umuhimu-wa.html
0 Response to "WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI"
Post a Comment