title : WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU
kiungo : WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU
WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingra Januari Makamba amesema watawasiliana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuangalia namna ya kupandisha hadhi Muungano kupitia mtaala wa somo la uraia ambalo linafundishwa shuleni.
Januari Makamba amesema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo moja ya swali liliuliza kuna mkakati gani wa kuwa na mtaala wa somo la Munungano ambalo litajikita kuelezea kwa kina historia ya Muungano uliopo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.
Hivyo Jauari ameliambia Bunge kuwa kwa sasa shuleni kuna mtalaa wa somo la uraia ambalo ndani yake wanafunzi wanafundishwa historia inayohusu muungano wetu lakini amesikia ushauri ulitolewa na wataufanyia kazi.
"Ni ushauri mzuri ambao umetolewa na mbunge kuhusu umuhimu wa somo la Muungano.Tumepokea ushauri huo na niwahakikishie wabunge tutaufanyia kazi kwa kuzungumza na Wizara ya Elimu na kisha tuone namna ya kufanya.Ni kweli historia ya muungano ikifundishwa shuleni itasaidia kuongeza uelewa,"amesema.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingra Alphaxad Kangi Lugola amesema hakuna kero za muungano bali kuna changamoto za Muunga na kuwaomba wabunge kuanzia sasa wawe wanasema changamoto.
Lugola ametoa kauli hiyo wakati anajibu maswali ya wabunge ambapo kila mmoja aliyepata nafasi alikuwa akiuliza swali kwa kuanza na kutaja kero za Muungano.Hivyo wakati anajibu maswali hayo Naibu Waziri huyo aliamua kufafanua kuwa ni vema wabunge wakafahamu hakuna kero bali kunachangamoto za Muungano.
Hivyo makala WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU
yaani makala yote WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/waziri-januari-azungumzia-somo-la.html
0 Response to "WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU"
Post a Comment